Você está na página 1de 3

NA MWANDISHI WETU

MJI wa Songea jana ulizizima kwa mapokezi makubwa ya


viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakiongozwa na
kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe.
Zitto, ambaye ameambatana na viongozi wengine wa juu wa ACT
akiwemo Mwenyekiti wa ACT Taifa, Anna Mghwira pamoja na
Katibu Mkuu wake Samson Mwigamba.
Viongosi hao walisili jana mjini hapa ambapo walilakiwa na
mamia ya wananchi wa mji wa Songea wakiongozwa na vijana wa
bodaboda zaidi ya 300.
Akihutubia mamia ya wananchi jana mjini Songea katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya
Malori Majengo, Zitto, alisema lengo la kuanza ziara mkoani
Ruvuma ikiwa kuenzi na kutekelza kwa vitendo azimo la Songea.
Alisema na hilo pia mkoa huo una historia ya ukombozi wa vita ya
majimaji iliyoanzia wilayani Kilwa na baadaye kuenea hadi
Songea.
Mbunge huyo wa zamani ya Kigoma Kaskazini, alisema kutokana
na hali hiyo ACT-Wazalendo wameanza ziara hiyo ili kupata
baraka za mababu wa ukombozi na si kushindana au kuviponda
vyama vingine vya siasa.
Alisema kitendo cha baadhi ya watu kufikiri kuwa ziara yake ina
lengo la mashambulizi si sahihi bali sasa ni changamoto kwa
wakazi wa mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanapanda viongozi wa
upinzani kama njia ya kustawisha demokrasia nchini.
Ruvuma ni Mkoa ambao hauna mbunge wa upinzani hata mmoja
na tumeona tutume salamu kwa umma huku lengo letu likiwa

likiwa kuingoa CCM madarakani na kwamba hatuna nia ya


kugambana na vyama vingine.
Wakazi wa Songea ni wajibu wenu kupima je pamoja na historia
ya ukombozi ambayo ACT-Wazalenzo tunaamini ndio misingi ya
ukombozi wan chi yetu je kukosa mbunge hata mmoja wa
upinzani ni sahihi, hili ni lazima tulikate na tufanye uamuzi huo
sasa hasa kuelekea Oktoba mwaka huu, alisema Zitto.
Akizungumzia Mkoa wa Ruvuma kama mmoja wa mikoa mitano
inayotegemewa kwa uzalishaji mkubwa wa chakula, alisema
pamoja na wakulima kuhangaika usiku na mchana lakini bado
hakuna juhusu za Serikali za kuwakomboa katika lindi la
umaskini ili wafurahie kilimo chao.
Alisema kwa muda sasa bei za mazao zimekuwa zikishuka lakini
bado Serikali imeshindwa kuwalipa wakulima Sh bilioni 13 za
mahindi bila kuwa na utaratibu madhubuti wa kulipa madeni
hayo.
Kwan chi zilizoendelea zimekuwa zikithamini juhudi
zinazofanywa na wakulima ikiwemo kuundiwa mfuko wa mazao,
ambao unafanya kazi ya kuhakikisha dhamani ya mazao
inalindwa.
Ikitoa bei ya mazao inashuka linakua jukumu la mfuko kulipa
fidia ya hasara kwa wakulima, ambapo hili huenda sambamba na
kuwepo kwa mfuko huo ambao.
Nasi ACT- Wazalendo tungependa kuonyesha sera yetu ya
hifadhi ya jamii ambapo kila mkulima awe na bima ya afya.
Mpango wetu ni kwamba kama mchango wa hifadhi ya jamii ni Sh
30,000 basi Serikali itamchangia mkulima Sh 10,000, alisema
Zitto .

Alisema kutokana na changamoto za wakulima wanataka


kuonyesha wana majawabu ambapo mkulima atatibiwa bure
akiwa na hifadhi ya jamii na uhakika wa bei kupitia mfumuko wa
bei katika hifadhi ya jamii.
Utafiti wa Shirikala la Kazi Duniani (ILO), wa mwaka 2013
unaonyesha kuwa nchi ambazo zimesambaza hiafdhi ya jamii kwa
wananchi wake wote zimeondoka kwenye umaskini kwa kasi na
ukiaji wa uchumi unaongezeka mara dufu, alisema Kiongozi
huyo wa ACT-Wazalendo.

Você também pode gostar