Você está na página 1de 2

TAARIFA YA KATA.

Kata zilizotembelewa ni sita ambazo ni;


1.
2.
3.
4.
5.
6.

Kabasa
Guta
Balili
Bunda
Kunzugu
Bunda stoo

Kata hizi zilitembelewa na Afisa kata wake Bw: Moses J. Mutash, na ifuatayo ni taarifa ya
yaliyojitokeza katika kila kata.
KABASA.
Afisa alitembelea kata hii tarehe 08/02/2012 lakini hakufanikiwa kuonana na mtendaji wa kata
wala kiongozi yeyote wa kata hii.Lakini alifanya juhudi na kupata namba ya simu ya mkononi ya
mtendaji wa kata( +255683359535) na kuongea nae kumweleza nia ya kufika hapo na kuomba
ushirikiano wake katika vita ya kupambana na wimbi la wahamiaji haramu. Kwa wakati huo
mtendaji huyo hakua na taarifa yoyote ya wahamiaji haramu ila aliahidi kutoa ushirikiano wa
dhati katika vita hii.
GUTA.
Kata hii ilitembelewa tarehe 08/02/2012, na Afisa alifanikiwa kuonana na Mtendaji wa kata hii
Bw. Majinji(+255784555578) na kujadili kwa kina masuala ya wahamiaji haramu lakini
mtendaji hakuwa na taarifa yoyote ya wahamiaji hawa, ila aliahidi kutoa taarifa kwa haraka
pindi tu atakapo pata taarifa yoyote juu ya suala hili.
BALILI.
Afisa alionana na mtendaji wa kata hii Bi: Esther (+255784638978) tarehe 08/02/2012 na
kujadili masuala ya uraia na wahamiaji haramu. Mtendaji aliona umuhimu wa masuala haya na
alimualika Afisa katika kikao cha wenyeviti wa mitaa ili kutoa mada kwa wenyeviti hao. Kikao
kilifanyika tarehe 10/02/2012 na Afisa alihudhuria na kutoa mada ya uraia na mapambano dhidi
ya wahamiaji haramu.Wajumbe wote walikiri kupata uelewa wa kina juu ya masuala hayo na
kuahidi kushirikiana kwa karibu zaidi na Idara.
BUNDA.
Katika hii imetembelewa zaidi ya mara nne bila mafanikio ya kumpata mtendaji wa kata, na kwa
taarifa zilizopatikana ni kwamba amesimamishwa kazi na bado Afisa hajafanikiwa kuonana na
aliyekahimishwa nafasi hiyo.

KUNZUGU.
Kata hii pia imetembelewa mara tatu bila mafaniko yoyote ya kumpata mtendaji wa kata wala
kiongozi yoyote.
BUNDA STOO.
Afisa alionana na mtendaji wa kata tarehe 14/02/2012, mtendaji huyo alitoa taarifa kuwa katika
kata yake hakuna wahamiaji haramu ila kuna familia mbili za Kiasia(Wahindi) ambao wanaishi
kwa vibali na kwa sasa wako katika mchakato wa kuomba uraia.Na kwa kumbukumbu za ofisi
yetu ni kwamba maombi hayo yako katika ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi.

Kata hizi zote ni kata ambazo zinauzunguka mji wa Bunda na zinafikika kwa urahisi
kwani haziko katika umbali mrefu.
Watendaji wa kata na viongozi wengine kwa sasa wanapatikana kwa shida kwa sababu
wamejikita zaidi katika shughuli za usimamizi wa ujenzi wa shule za sekondari.
Jitihada zinaendelea kufanyika hasa kwa kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na
kusambaza vitabu maalum vya kuandikisha wageni.katika kila kata, japokuwa bado kuna
upungufu wa vitabu hivyo.

Você também pode gostar