Você está na página 1de 6

TAARIFA YA ZIARA YA KATA NA UKAGUZI WA MAENEO MENGINE-BUNDA.

UTANGULIZI:
Ziara hii ilifanyika kwa siku mbili za tarehe 24/04/2012 na 25/04/2012 katika kata zote za tarafa
ya Kenkombyo na katika maeneo ya mbuga ya Serengeti yaliyo ndani ya wilaya hii.Kazi hii
ilifanywa na maafisa watatu(3) pamoja na dereva mmoja(1) kutoka ofisi ya mkoa kama majina
yao yanavyoonekana hapa chini.
1.
2.
3.
4.

MOSES J. MUTASH-Mkaguzi
MASIJA BUCHAFWE-Mkaguzi
WALTER E. LEMA-Konstebo
WARYOBA MAGIGE-Dereva

ZIARA YA KATA-24/04/2012
1. KATA YA BUTIMBA.
Katika kata hii tulionana na mtendaji wa kata Bi.Christabell(0685421361) na kutupa taarifa
kuwa katika kata yake hana taarifa yoyote ya kuwepo wahamiaji haramu, ila ameandaa mkutano
wa hadhara kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya suala la uraia na mapambano dhidi ya
wahamiaji haramu. Pia amepanga kuwa na utaratibu wa kuzunguka kila kijiji ndani ya kata yake
ili kukusanya taarifa yoyote ya kuwepo kwa wageni.
Aidha tulitembelea kiwanda cha S&C GINNING CO. L.T.D na kukagua vibali vya wafanyakazi
wasio raia. Kiwanda hiki kina wafanyakazi saba raia wa India wenye vibali daraja B
vilivyohai,kama ilivyoainishwa hapa chini.

SN

JINA KAMILI

CHEO/WADHIFA

NAMBA
YA
KIBALI

MUDA WA
MWISHO WA
UHAI WA
KIBALI

Ramasubramanyam
Cherukori

General Manager

099254

27/01/2013

Umakant Mahaden Kolaki

Factory Manager

088928

24/06/2013

Ambrish Pravinchibhai
Solanki

Factory Manager

088977

24/06/2013

Viralkumar Jayeshkumar

Business

088893

15/02/2013

Rabia

Development
Manager

Amin Umarbhai Darjada

Techinician

103097

13/09/2012

Sayanja Kumar Mukherjee

Business
Development
Manager

099003

07/02/2013

Ghulam Minai Warsi

System Analyst

08020

17/11/2013

NB: Taarifa ya return of employment of non-citizen tuliyoagiza iandaliwe itafafanua zaidi.


Vilevile tulimuagiza mtendaji kuweka utaratibu wa kuwa anatembelea kiwanda hicho mara kwa
mara ili kupata taarifa sahihi pindi zinapohitajika.
2. KATA YA KASUGUTI.
Tulionana na mtendaji wa kata hii Bw. Bajumaa(0784-596358) na kutupa taarifa kuwa Diwani
wa kata hii Bw. Flugence Kanazi-0787-092694 anasadikiwa kuwa ni raia Rwanda kwa asili
yake, hivyo anaomba ufanyike uchunguzi wa kina juu ya suala hili ili kuondoa utata kwa
wananchi . Suala hili tumelifikisha kwa Afisa Uhamiaji Wilaya kwa hatua zaidi.
Pia alitupa taarifa kuwa siku chache baada ya semina aliyoipata ya uraia na mapambano dhidi ya
wahamiaji haramu alifanya mkutano wa hadhara na kuwaelimisha wananchi suala la uraia na
mapambano dhidi ya wahamiaji haramu.
3. KATA YA NYERUMA.
Mtendaji wa kata hii hakupatikana kwani tulipata taarifa kutoka kwa kaimu wake Bw. Baraka
Lumbaga( mtendaji wa kijiji cha Kasahunga) kuwa anaumwa. Mtendaji huyu wa kijiji alitupa
taarifa ya kuwepo kwa raia wawili wa Kenya walioolewa na watanzania,(majina yao
yamaeorodheshwa hapa chini).
1) Bi. Magreth-Anaishi na Mwl. Joseph Okuku Washngton wa Shule ya
Sekondari Nyeruma.
2) Bi. Alice Auwori
mfanyabiashara.

Modok-Ameolewa

na

Bw. Modekay

Miran-

Tulifanya jitihada za kuwapata kinamama hawa lakini hatukufanikiwa kwani kwa wakati huo
hawakuwepo kijijini hapo.Lakini tulionana na wanaume husika na kufanya nao mahojiano ya

kina na kubaini kuwa wanaishi na kinamama hao kinyume cha sheria kwani hawana vibali
vyovyote . Baada ya mahojiano hayo tuliwaagiza wafike ofisini siku ya tarehe 27/04/2012 kwa
mahijiano zaidi na kupatiwa utaratibu wa kufuata ili kuishi kihalali na kinamama hao.
Mwl Washngton alifika ofisini na kujaza fomu ya hojaji ili uafanyike uchunguzi zaidi juu ya
uraia wake(fomu zitatumwa ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi),lakini pia alipewa utaratibu wa
kufuata ili kuhalalisha ukaazi wa mwenza wake.
Bw. Modekay hajafika ofisini mpaka sasa,unafanyika utaratibu wa kumkamata.
4. KATA YA NAMHULA.
Mtendaji wa kata Bw. Boniphas Manyonyi(0784-944811) alitupa taarifa kuwa ameendaa
mkutano wa hadhara tarehe 26/04/2012 utakaohusisha asasi mbalimbali na wanachi kwa ujumla
akiwa na lengo la kuhamasisha mapambano dhidi ya wahamiaji haramu na suala la utoaji taatifa
kwa wakati katika vyombo husika.Vilevile alieleza kuwa katika vijiji vya Karukekere na
Muranda kuna wakenya wengi, hivyo panahitajika nguvu ya ziada ikiwezekana kufanya mkutano
wa hadhara katika vijiji hivyo
Tulimuagiza katika mkutano huo awasisitizie sana watendaji wa vijiji hivyo juu suala hili.
5. KATA YA IRAMBA.
Mtendaji wa kata Bw. Fares Mahuku (0784-908148) alitupa taarifa kuwa ameshafanya vikao
mbalimbali na viongozi wa vijiji juu ya suala la wahamiaji haramu.Pia akatupa taarifa ya
kuwepo raia mmoja wa Kenya Bw. Ogengo Ogada katika kijiji cha Mgara.Tulifika kijijini hapo
na kuonana na mtajwa na kufanya nae mahojiano na kukiri kuwa yeye ni mkenya aliyeingia
nchini tangu mwaka 1953 na hajawahi kafanya taratibu zozote za kuhalalisha ukaazi
wake.Tulimuagiza kufika ofisini tarehe 27/04/2012, alifika na kupewa utaratibu na akaanza
mchalato wa kuomba kibali cha ukaazi(ombi lake litafikishwa ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi)
Pia tulimueleza kwamba katika familia yake kuna idadi ya watu watano wanaohitajika kufuata
utaratibu huo, hivyo awaeleze na kuwahimiza kufanya hivyo kwa haraka.

ZIARA YA MAENEO MENGINE.25/04/2012.

A. NYANZA FARMING CO. LTD


Ukaguzi ulifanyika na kukuta raia wanne(04) wa India wenye vibali daraja B vilivyohai kama
inavyoainishwa hapa chini.

SN

JINA KAMILI

CHEO/WADHIFA

NAMBA YA
KIBALI

MUDA WA
MWISHO WA
UHAI WA
KIBALI

Vishalkumar Vinubhai Patel

Farm Manager

0612417

01/03/2013

Jaspal Singh

Heavy Plant
Manager

099499

06/10/2013

Patel Vinodkumar
Ramjimbhai

Farm Manager

0612420

13/02/2013

Inderjit Singh Dharam Singh

Plant Manager

0612443

13/02/2013

B. MBUGA YA SERENGETI.
Katika mbuga hii tulipanga kufika katika maeneo yafuatayo:
1) KENSINGTON TENTED CAMP
2) KIRAWIRA LUXURY TENTED CAMP
3) MBALAGET TENTED CAMP
4) GRUMET TENTED CAMP
KENSINGTON TENTED CAMP
Hatukwenda kabisa baada ya kupata taarifa za awali kuwa camp hiyo ilishafungwa.
KIRAWIRA LUXURY TENTED CAMP.
Tulifika na kukuta kuna mfanyakazi mmoja raia wa Kenya B w. Jonathan Cheres-Camp Manager
akiwa na kibali daraja B Na. 092778 kinachoisha tarehe 19/07/2012.

MBALAGET TENTED CAMP

Hatukufanikiwa kufika kwa sababu ya ubovu wa barabara.


GRUMET TENTED CAMP
Hatukufika kwa sababu ya ubovu wa barabara.

CHANGAMOTO/VIKWAZO
I.

KUSUBIRI KIBALI CHA KUINGIA MBUGANI KWA MUDA MREFU

Hiki kilikuwa kikwazo kikubwa kwetu kwani tulitumia muda mrefu sana katika geti la Ndabaka
tukisuburi ruhusa ya kuingia mbugani kwa sababu tuliyopewa kwamba hatukuwa tumetoa taarifa
ya awali kwamba tutakua na safari hiyo kwa ajili ya kazi. Hili tunaliona kama litaendelea kuwa
kikwazo kikubwa zaidi katika utendaji kazi wetu kama halitatafutiwa ufumbuzi na njia mbadala
ya kukabiliana nalo.Kwani kwa wakati mwingine inaweza kupelekea hata kukosa kile
kilichokusudiwa baada ya kuzagaa kwa taarifa katika maeneo mbalimbali ya mbuga kuwa kuna
maafisa wanaingia mbugani,kwa maana nyingine hii inaondoa usiri wa kazi husika.
II.

UBOVU WA BARABARA

Hii ilipelekea kusafiri ndani ya mbuga kwa tabu sana na kwa muda mrefu kwa sababu ya
barabara kujaa maji, tope jingi na mashimo mengi na kupalekea kushindwa kufika katika maeneo
tajwa hapo juu.
III.

GARI KUHARIBIKA

Gari tulilokuwa tukitumia LandRover Defender Na.STJ 1662 liliharibika tukiwa mbugani umbali
kama wa kilometa 2 kutoka Kirawira Tented Camp eneo ambalo lilikuwa ni la hatari kwa
usalama wa maisha yetu kwani ni eneo lililo na wanyama wengi wa hatari hususan Simba. Hii
ilipelekea kulala huko kinyume na matarajio yetu.
MAPENDEKEZO.
Tunaomba uongozi wetu ufanye utaratibu wa kuonana na uongozo wa Mbuga ya Serengeti na
kujadili uwezekano wa kuweka utaratibu mwingine wa utoaji vibali kwa watumishi wa vyombo
vya ulinzi na usalama pindi panapokuwa na hitaji la kufanya kazi ndani ya mbuga hiyo, kwani
kazi hizo hufanyika kwa maslahi ya serikali na watanzania wote kwa ujumla.
Tunaomba pale itakapowezekana tupatiwe tena gari ili tuweze kufika katika maeneo mengine
ambayo hatukuweza kufika,hususan katika vijiji vya Karukekere na Muranda ambavyo vinahitaji
msisitozo zaidi katika mapambano dhidi ya wahamiaji haramu.

SHUKRANI
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa uhamiaji mkoa kwa kutoa idhini ya kutumia gari
tajwa na kuwezesha kazi yetu kwa kiwango hicho kilichofikiwa.
Shukrani za pekee tunazitoa kwa uongozi wa Kirawira Luxury Tented Camp kwa msaada
mkubwa waliotupatia baada ya kuharibikiwa na gari.Uongozi huu ulitupatia hifadhi ya miili yetu
na huduma mbalimbali hususan chakula na kutusaidia usafiri wa kutoka mbugani mpaka kufika
Bunda mjini,Mungu awabariki sana.
MATARAJIO
Tunatarajia kufanya kazi kwa moyo,nguvu,uaminifu na hari katika kendeleza mapambano dhidi
ya wimbi la wahamiaji haramu hasa kwa kuhakikisha tunatembelea kata zote ndani ya wilaya
hii.Lakini hili litawezekana kwa kuwa na usafiri wa uhakika.

Naomba kuwasilisha.

MOSES J. MUTASH -MKAGUZI

Você também pode gostar