Escolar Documentos
Profissional Documentos
Cultura Documentos
tz
Sauti ya Waislamu
ISSN 0856 - 3861 Na. 1055 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Uk. 2
Sisi ni Waislamu Chwaka wataka Rais Kikwete kwanza - Waziri kuirejeshea Zanzibar mamlaka Wampa changamoto nzito Dr. Shein
MUHIMU hapa ni kuona kwamba tumekuwa kuwa na Dini ya Kiislamu kwa karne nyingi sana na sasa kila mtu anajua kwamba Uislamu si dini tu peke yake, lakini imechimba zaidi hata katika tabia, silka na hulka zetu. Waislamu tumeungana zaidi kwa lugha yetu moja na kuwa sote ni wamoja. Wajibu wetu wa kwanza ni kuunganisha umoja wetu huu (wa Kiislamu) kwa misingi nilioieleza. (Mh. Abubakar Khamis Bakary-Soma Uk. 13) Na Mwandishi Wetu WANANCHI wa kijiji cha Chwaka, Kusini Unguja wamewaomba Rais Jakaya Kikwete na Dk Ali Mohamed Shein, kushughulikia suala la Zanzibar kurejeshewa mamlaka yake kamili kama ilivyokuwa kabla ya kuungana na Tanganyika. Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Katiba Zanzibar (BAKAZA) wakati likitoa elimu ya Katiba kwa wananchi wa kijiji hicho. Huo ni mfululizo wa Baraza Inaendelea Uk. 4
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
AN-NUUR
AN-NUUR
MAONI YETU
Maulid itukomboe
KUANZIA jana usiku, Waislamu sehemu mbalimbali nchini na maeneo mengine duniani, wamekuwa katika sherehe za Maulidi ya Mazazi ya Mtume (saw). Wa k a t i S h e r e h e h i z i zikiadhimishwa, yapo mambo inabidi Waislamu kujiuliza na kuona ni vipi wananufaika na ujio wa Mtume Muhammad (s.a.w). Kwanza ni kuwa, kwa muda mrefu sasa Waislamu wa nchi hii wamekuwa na madai na hata kulalamika kwamba wanabaguliwa na kudhulumiwa haki zao. Wanadai kuwa kumekuwa na mfumokristo ambao uliasisiwa toka wakati wa ukoloni ambao ndio umekuwa sababu ya wao kudhulumiwa haki zao kama wananchi. Kwa upande mwingine w a n a d a i k u w a Wa k r i s t o wamehodhi fursa za elimu, ajira na madaraka serikalini na katika taasisi za umma kutokana na upendeleo wanaopewa chini ya mfumokristo. Kwa maelezo yao wenyewe, Waislamu wa nchi hii wanajiona kama raia daraja la pili. Swali ni je, mafundisho ya Uislamu, mafundisho ya Mtume wanayesherehekea uzao wake, yanawasaidia vipi Waislamu kujinasua na hali hii? Kama kuja kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kumetajwa kuwa ni Rehma kwa walimwengu, je, Rehma hii, inawasaidiaje Waislamu wanaodai kubaguliwa na kuonewa? Katika jumla ya mafundisho aliyokuja nayo Mtume (s.a.w) ni kuwa Waislamu wasidhulumu na wala wasikubali kudhulumiwa. Je, hii hali ya kulalamika miaka yote hii kwamba wnaabaguliwa na kudhulumiwa, ni katika Uislamu? Mbona inakuwa kinyume na mafundisho ya Mtume? Kwa nini Waislamu waendelee kulalamika wakati dini yao inawakataza wssikubali kudhulumiwa? Je, dhulma itaondoka kwa kulalamika? Tuseme kuwa yapo masuala ya kisera ambayo yamekuwa yakiwaletea Waislamu nchini athari kubwa na mbaya kiasi cha kuuingiza umma katika mateso makubwa. Kwa hakika Waislamu kwa sasa wana kila sababu ya kujikita zaidi katika masuala hayo ya kisera ili kuhakikisha wanakuwa huru katika Uislamu wao dhidi ya sera zinazotawala nchini. Waislamu wanakabiliwa na tatizo la kukosa uhuru wa kuabudu. Uhuru wa kuwa na Jumuyia raki za kimaendeleo, uhuru wa kuitumikia dola inayokuwa madarakani kutokana na kufunikwa na mfumokristo nk. Kipindi hiki cha kusherehekea uzao wa Mtume (s.a.w) ndio wakati hasa wa kutafakari, ni hatua zipi za kuchukua kuhakikisha kuwa katika yale wanayopalalamikia angalau ikija maulidi nyingine mwakani, basi waweze kusema kuwa hili na lile limeondoka Hivi sasa kuna hizi harakati zinaendelea za Katina mpya, ni kipindi ambacho tunaona kila Muislamu anatakiwa kufuatilia kwa karibu mchakato huu wa katiba kuhakikisha kwamba Waislamu wanakomboka katika kitanzi cha kukosa uhuru wa kuabudu kulingana na imani yao kwa kigezo cha katiba. Kama ni mahakama ya kadhi, kujiunga na taasisi za kijamii na kiuchumi kama OIC, kuwa huru siku za ibada ya Ijumaa, kuwa huru kuvaa kwa heshima hata katika maeneo ya kiserikali, (Hijab, koa n.k., kuwepo mfumo huru halali wa kiutendaji serikalini, kupewa ruzuku kama watu wa inami nyingine nk. Haya ni masuala ya msingi ya kufanyiwa kazi kipindi hiki cha mchakato wa mabadiliko ya katiba. Hata hivyo, jambo muhimu sio kuwekwa katiba au sharia kwani hata katiba ya sasa inapinga ubaguzi. Muhimu kwa Waislamu ni kujenga ile dhamira ya kukataa kuonewa na wakawa tayari kulisimamia hilo na kwa gharama yoyote. Hata kama itakuwepo katiba nzuri, lakini Waislamu wenyewe wakawa hawa hawa ambao wanaona dhulma ya wazi katika taasisi kama ya Baraza la Mitihani, lakini hawaonekani kuchukua hatua madhubuti na makini kuondoa dhulma hiyo, huna vya kuwasaidia. Hao wataendelea kudhulumiwa na kuonewa hata kukiwa na katiba nzuri kiasi gani. Hata kama kutakuwa na katiba nzuri kiasi gani, lakini Waislamu wenyewe wakawa hawa hawa ambao mtu akiwa mwanasiasa, msomi, mfanyabiashara aliyefanikiwa na asa wa serikali, anajiona hana la kupigania Uislamu na Waislamu ila huona kuwa hilo ni jukumu la wanaharakati, bado itakuwa kazi ngumu kwa Waislamu wa nchi hii kuepukana na dhulma. Ni matarajio yetu kuwa tutasherehekea Maulid huku tukitafakari jinsi Mtume (s.a.w) alivyowakomboa Waislamu kutoka makucha ya madhalimu wa Makkah ili nasi tupate kujikomboa.
Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN). Tunasikitika kuwa yeye hayupo nasi kushuhudia mafanikio hayo. Hata hivyo kumbukumbu zake zitaendelea kubaki mioyoni mwetu, na harakati za ukombozi zitaendelea hadi kufikia uhuru kamili wa nchi yetu na hatimae kukubalika kwa Palestina kama mwanachama kamili wa UN Balozi Abujaish alisema President Arafat na chama cha PLO walikuwa karibu sana na taifa la Tanzania na chama cha CCM. Wapalestina leo wana faghari kwa uhusiano huu wa kihistoria baina ya mataifa yetu na wananchi
Balozi wa Dola ya Palestina, Dr Nasri Abujaish (kushoto) na Bw Richard Chengula aliyemuwakilisha Meya wa Kinondoni Mheshimiwa Yusuf Mwenda.
uhusiano wa kiraki baina ya Tanzania na Palestina. Alisema barabara hiyo itawakumbusha wananchi k u w a Ta n z a n i a i l i k u w a miongoni mwa nchi ya kwanza kuitambua Dola ya Palestina. Naye Balozi wa Dola ya Palestina, Dr Nasri Abujaish alisema alifurahi sana na kuwashukuru wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kuipa barabara hiyo jina la Bw Yasser Arafat ambaye alikuwa mwanzilishi wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Rais wa kwanza wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina na Rais wa kwanza wa Dola ya Palestina. Akasema, sababu muhimu zaidi ya uamuzi huu ni Yasser Arafat hapa nchini Tanzania. Ni matumaini yetu kuwa hatua hizi tulizochukua zitaendeleza na kuimarisha kumbukumbu za viongozi wetu wakuu hawa ili waendelee kukumbukwa na vizazi vijavyo. Balozi alisema Wapalestina watamkumbuka Arafat kwa vile ndie aliyeanzisha vuguvugu la ukombozi wa Palestina kutokana na uvamizi wa Israel. Arafat atakumbukwa pia kwa sababu anawakilisha dira yetu ya kitaifa na ukombozi wa taifa letu la Palestina Hivi leo moto aliouwashaYassir Arafat umezaa matunda kutokana na kukubalika kwa Dola ya wetu. Ni matumaini yetu kuwa uhusiano huu utaendelezwa na kuimarishwa, aliongeza Ni kwa sababu uhusiano huu umetokana na mshikamano wenu wa dhati na Wapalestina ambao wanapambana na uvamizi na ukandamizaji wa Israel nchini mwao. Kwa kweli nyinyi Watanzania mmechukua msimamo huu dhidi ya ukoloni wa Israel sawa na mlivyofanya wakati ule wa utawala wa makaburu kule Afrika Kusini. Kwa hili tunawashukuru sana kwa moyo wetu wote, alimalizia Balozi Abujaish. (Habari hizi ni kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina Tanzania 24 January 2013.)
3
Na Alghaithiyyah Zanzibar, RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, ameomba kupatiwa hati halisi (Original) ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo imetiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume. Ombi hilo la Karume limekuja kufuatia utoaji wake wa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, makamo Mwenyekiti Assa Rashid na wajumbe wengine aliyokutana nayo juzi nyumbani kwake Mjini Unguja. Karume alisema yeye hana hati ya Muungano na hajawahi k u i o n a n a i w a p o Tu m e hiyo inayo hati hiyo, basi angeomba kupatiwa kwani ni Wazanzibari wengi wanahitaji kuiona hati hiyo ambayo ni mkataba kati ya nchi mbili zenye mamlaka kamili kila moja na zilizoungana mnamo mwaka 1964 kila nchi ikiwa huru. Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya tume hiyo, kimesema Karume mbali ya kutaka kupatiwa hati ya Muungano lakini pia alisema anaunga mkono kuwepo kwa Muungano wa Mkataba ambao kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili na kisha
Habari
AN-NUUR
RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume. kufuatia huo na mfungamano wa mkataba ambapo alisema Zanzibar kwa takriban miaka 50 sasa imekuwemo katika Muungano lakini imekuwa hainufaiki kiuchumi ndani ya Muungano huo. Aidha Karume alisema yeye yupo tayari kuongoza kipindi cha mpito iwapo kutakuwepo na kipindi hicho kutoka Muungano huu uliopo
MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad. na kuingia wa Maktaba pale alipoulizwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Salim Ahmed Salim ambaye alionesha khofu yake na uzoefu wa chaguzi zinazofanyika nchini kwamba zinakuwa na machafuko. Karume alisema hakuna machafuko yoyote yatakayoweza kutokezea katika kipindi hicho cha mpito na iwapo Rais aliyekuwepo madarakani hataweza
Habari
AN-NUUR
TUME ya mabadiliko Katiba mpya, imeelezwa kuwa Baraza la Mapinduzi halikushauriwa wala kushirikishwa katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ulioundwa Aprili 26, 1964. Wanasiasa wakongwe waliyokuwa katika Serikali ya Mapinduzi, wakati wa kuundwa kwa Muungano huo, Bw Salum Rashid na Bw Hassan Nassor Moyo waliiyambia Tume hiyo, walipokuwa wakitoa maoni yao Maisara, mjini Zanzibar. Katika maoni yao walisema: Tangu awali katika kuundwa Muungano, kulikosekana uhalali, licha ya kuwa umedumu kwa miaka hamsini huku kukiwa na malalamiko kadhaa ya wananchi. Wa k i z u n g u m z a k w a pamoja, Wanasiasa hao waliunga mkono kuwepo kwa Muungano, lakini walishauri mfumo mpya wa Muungano wa Mkataba, ili kila nchi kuwa na mamlaka yake kamili: Kwa hali ilivyo miaka 50 ya Muungano kushindwa kutatua mambo mbali mbali, mfumo pekee unaofaa kwa sasa na kwa kizazi hiki ni Muungano wa Mkataba. Utaratibu wake utajulikana baadae, walisema Wanasiasa hao. Bwana Nassoro Moyo alisema Serikali ya Muungano, isiogope maoni ya wananchi kwani kwa takriban miaka 50 matatizo ya Muungano yameshindwa kutatuliwa na njia pekee kwa sasa ni kukubali kubadilisha mfumo wa Muungano huo. Tukiwa na mfumo mpya wa Muungano, utakwenda sambamba na wakati huu ambao idadi ku bwa ya wananchi wameamka na kuona kuna matatizo katika Muungano wetu, alisema Mzee Moyo. Mzee Moyo alikuwa Waziri wa kwanza wa Sheria wa Serikali ya Muungano, na Bwana Salum Rashid alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi. Kwa pamoja, wazee hao wakongwe wa siasa za Zanzibar, walishauri kuwepo kwa Muungano lakini walisisitiza, ili kuimarisha Muungano kwa nchi zote mbili, ni kusikilizwa kwa maoni ya wananchi ambao wanataka aina mpya ya Muungano wa Mkataba. Sisi ndiyo tulikuwa
DKT. Salmin Amour na dhamana wakati ule na tulitakiwa tuunganishe Serikali kwa kuimarisha udugu na kuimarisha uchumi wetu, bahati mbaya sasa kuna kero, mimi siziiti kero naita ni matatizo, ni wakati wake kuondoshwa, alisema na kubainisha: Msimamo wangu ni Serikali ya Mkataba na ndiyo ninavyoamini na naamini kwamba huu muungano tulionao ni Muungano wa Mkataba, hili siyo jambo jipya, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume walitia saini ya Mkataba, hili sio jambo jipya, alisisitiza Mzee Moyo. Moyo alitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani, ili Rais wa Zanzibar aendelee kuwa Makamo wa Kwanza w a R a i s w a Ta n z a n i a , akimaanisha Muungano huo ni wa Tanganyika na Zanzibar. Naye, Katibu Mkuu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Mzee Salum Rashid ambaye alikuwa Dar es Saalm na Mzee Karume siku ya kusainiwa Mkataba wa Muungano, alisisitiza kuwepo kwa Muungano wenye maslahi kwa wananchi wa nchi zote mbili. Serikali ya Muungano isiwe na woga wa kuvunjika kwa Muungano. Hilo sio jambo kubwa na wala siyo jambo geni, baadhi ya nchi za Afrika ziliwahi kuungana, na Muungano ukavunjika, alisema na kufafanua zaidi akisema: Sioni jambo zito kuvunjika kwa Muungano, mbona Muungano wa Senegal na Gambia ulivunjika na wote walikuwa ni wanachama wa Umoja wa Afrika na hakuna jambo lolote lililotokea, alisema Bw Salum Rashid. Alisema wananchi wanaotaka Muungano wa Mkataba, hawamaanishi kuvunja Muungano, bali
DKT. Amani Karume wanataka mfumo mpya wa Muungano ili kuirudishia Z a n z i b a r, m a m l a k a n a madaraka yake kamili. Alisema ifahamike kwamba, kuwa nje ya Serikali siyo sababu ya kuwa ni fursa ya kuzungumza hayo, lakini wakati ule likizungumzwa suala la Muungano, ilikuwa inaonekana ni uhaini. Alisema kwa sasa haiwezekani tena kuburuzwa na hasa vijana. Hivyo matumaini yake kwa tume hiyo ni makubwa. Naamini watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa na maoni ya wananchi ambayo w a m e y a t o a k w a Tu m e , yatatekelezwa, alisema Bw Salum Rashid. Alisisitiza kuwa Muungano wa Mkataba ndiyo sahihi kwa sasa na hakuna sababu ya viongozi kuogopa hilo, Wazanzibari na hasa vijana wanataka nchi yao kuwa na mamlaka kamili. Mzee Moyo na Rashid, wote wawili kwa pamoja wamewatoa hofu Wazanzibari kuhusu utendaji wa Tume hiyo, na walisema wanaiamini kwamba itafanya kazi yake kwa uadilifu, bila upotoshaji. Tume hiyo inayongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume, Assa Rashid tayari imeshachukuwa maoni ya baadhi ya viongozi wakuu, pamoja na Marais wastaafu wa Serikali ya Zanzibar. Viongozi waliyokwisha toa maoni yao ni pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu Dk Salmin Amour, Dk Amani Abeid Karume na baadhi viongozi wengine wa Serikali ya Zanzibar.. Wakati huo huo Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe Amani Abeid Amani Karume amesema kwamba wakati wa siku za mwanzoni, Muungano
Bw Salum Rashid ulikuwa wa heshima na usawa kati ya Zanzibar na Tanganyika lakini kadiri siku zinavyokwenda unachukua sura ya nchi moja -Tanganyika kuuhodhi Muungano huo dhidi ya Zanzibar. Akasema akiwa Rais kwa kipindi cha miaka 10 ameshuhudia mengi dhidi ya maslahi ya Zanzibar. Mheshimiwa Dr. Karume amesema hayo wakati alipokutana na Tume ya Jaji Warioba na kutoa maoni yake juu ya Katiba Mpya. Katika maoni yake Dr. Karume amesema kuwa hizi ni zama mpya za uwazi na ukweli na kwa hali iliyokia sasa, hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi Zanzibar na Tanganyika kurejesha mamlaka yake (sovereignty) kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kupitia Muungano wa Mkataba kati yao. Naye Rais Mstaafu aliyemtangulia Dr. Amani, Mheshimiwa Dr. Salmin Amour, maarufu Komandoo, katika maoni yake ameieleza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba anataka kuona Zanzibar na Tanganyika kila moja ikiwa ni nchi yenye mamlaka kamili ndani na nje na kisha zishirikiane kwa mfumo wa ushirikiano kama ule uliopo baina ya nchi za Afrika kupitia Umoja wa Afrika (AU). Dk. Salmin Amour amesema msingi wa umoja wa nchi za Afrika umetokana na mashirikiano kati ya vyama vya ukombozi chini ya PAFMECA. Akasema Umoja wa Vyama vya Ukombozi vya Afrika Mashariki na Kati (PAFMECA) ulitambua haja ya nchi za Afrika kuungana baada ya uhuru, lakini kwa msingi wa kuheshimu mamlaka ya kila nchi (sovereignty) na mipaka yake.
Bw Hassan Nassor Moyo Hivyo, akataka mahusiano mapya kati ya Zanzibar na Tanganyika yazingatie msingi huo ambao ndiyo pia uliojenga misingi ya Umoja wa Afrika (African Union). Kwamba kama ni muungano, basi Tanganyika na Zanzibar wakutane katika Umoja wa Afrika. Kwa upande mwingine baadhi ya wananchi wameponda hoja za wanaozungumzia udogo wa Zanzibar kwamba ni kikwazo cha kusimama kama nchi wakisema kuwa wachukue mfano wa Cape Verde ambayo hivi karibuni katika mchezo wa mpira imecheza na kutoka sare na nchi kubwa ya Afrika ya Kusini. Cape Verde ni nchi ndogo yenye watu wasiofika laki sita, lakini juzi hapa katika michezo ya Afrika imecheza ikiwa na bendera yake na kutoka sare na Afrika ya Kusini nchi kubwa yenye watu zaidi ya milioni 52. Amesema mtoa maoni mmoja. Watizame Singapore, nchi ndogo kuliko Zanzibar na ilikuwa imeungana na Malaysia, lakini ilijitenga na sasa ipo mbali kimaendeleo, huwezi kuilinganisha na Unguja iliyo katika muungano, kwa hiyo hoja sio udogo wa nchi wala muungano, ni dhamira na mipango ya nchi katika kujiendeleza, sisi Zanzibar dhamira tunaweza kuwa nayo, lakini hiyo mipango tunaiweka na kuitekeleza vipi chini ya makucha ya muungano wakati hata OIC tulikatazwa kujiunga ili tusinufaike na misaada ya Benki ya Kiislamu isiyo na riba. Amesema mwananchi huyo ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
MSIKITI wa al Aqsa
wa kutekelezwa mipango miovu ya kutaka kukiharibu kikamilifu kibla hicho cha kwanza cha Waislamu. Wazayuni wanatumia njia tofauti za kuuharibu msikiti wa al Aqsa ikiwa ni pamoja na kuchimba mashimo mengi na njia za chini ya msikiti huo mtukufu na kando kando yake. Vitendo hivyo kwa kweli vina lengo la kuzidhoosha kuta za msikiti wa al Aqsa ili eneo hilo takatifu liweze kuharibika kwa mtikisiko mdogo tu wa ardhi au mripuko. Hivi karibuni ilifichuliwa kuwa, moja ya mashirika ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni linalojulikana kwa jina la Kaj lilifanya kikao na marubani wa Kizayuni kuwashawishi wadodoshe bomu kwenye msikiti huo. Tangu kuundwa utawala huo pandikizi katika ardhi za Palestina hadi hivi sasa, msikiti mtukufu wa al Aqsa umeshashambuliwa mara kadhaa na Wazayuni. Mwaka 1969 Wazayuni wenye misimamo mikali wakiongozwa na Dennis Michael Rohan, waliuchoma moto msikiti huo wa kihistoria, hatua ambayo iliratibiwa na makundi ya watalii kwa ushirikiano na viongozi wa Tel Aviv. Katika tukio hilo, mita mraba zisizopungua 200 za dari ya msikiti huo ziliharibiwa na kuanguka kabisa, pande tano za kuba la msikiti huo ziliungua na mimbari yenye thamani kubwa iliyojengwa miaka 800 iliyopita, iliteketea kabisa kwa moto. Huku mji wa Baitul Muqaddas na msikiti wa al Aqsa ukikabiliwa na duru mpya ya vitisho na njama za utawala wa Kizayuni, fikra za walio wengi duniani wanaitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti na za haraka za kupambana na utawala huo, wakiamini kwamba, kucheleweshwa suala hilo kutaifanya Israel kuendelea na hatua zake hizo za uharibifu bila ya woga.
URUSI imeanza kufanya mazoezi makubwa ya jeshi lake la majini katika bahari za Mediterranean na Bahari Nyeusi, karibu na Syria ambayo inakabiliwa na mashambulizi ya magenge ya waasi. Mazoezi hayo yameelezwa kuwa ni makubwa zaidi kufanywa na Jeshi la Majini la Urusi kwa miongo kadhaa. Taarifa rasmi ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa, mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika katika utaratibu wa vikosi vya ulinzi vya Urusi wa mwaka 2013, wa kujiimarisha kiulinzi na kuzingatia zaidi suala la kufanya kazi kwa pamoja vikosi vya nchi hiyo, kutoka manowari zake mbalimbali zinapokuwa katika eneo la maji la mbali. Mazoezi hayo ya Jeshi la Majini yataendelea hadi Januari 29 na kufanya majaribio ya silaha na mbinu tofauti za kivita. Urusi imekuwa ikizilaumu nchi za Magharibi kwa kuchochea mauaji na uasi nchini Syria, na kusababisha kushuhudiwa machafuko tangu katikati ya Machi 2011. Raia wengi na maasa usalama wa serikali ya Syria wameuawa katika machafuko hayo.
Moscow. Bw. Lavrov amesema, hakuna sababu zozote za kuwepo uadui wa serikali za Uturuki na Qatar dhidi ya serikali ya Damascus, kwani nchi hizo zilikuwa na mahusiano mazuri na serikali ya Syria. Lavrov amesisitiza kuwa, mgogoro wa Syria kamwe hauwezi kumalizwa kwa njia za kijeshi na kwamba, njia pekee ya kutatua mzozo huo ni kuketi kwenye meza ya mazungumzo.
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Baadhi ya Viongozi waliotoa mada mbali mbali meza kuu wakiwa katika Kongamano la kidini lililoandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Kimisr Markaz cha jijini Dar es salaam kongamano hilo lilifanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na washiriki 180 hivi karibuni.
mifano michache iliyoenea na ni mashuhuri masikioni mwa wasikilizaji pale alipoingia mtume kuikomboa maka na kuwasamehe watu wa makka ambao walimuadhibu yeye na masahaba zake. Hakuongeza la kusema isipokuwa aliwambia Enyi watu wa makka hivi mnadhani mimi nitakufanyeni nini nyinyi? wakasema kheri
ndugu mwema na mtoto wa ndugu mwema Akasema Nendeni na nyinyi mupo huru (S.A.W)
Zakka ya mwaka huu imelenga kuwasaidia kina mama Wajane Masikini/ Mafukara 15 na Wanafunzi 15 wasio na uwezo. Kwa mawasiliano zaidi piga simu: 0716 776226, 0713 208585, 0754 434968. Wote mnakaribishwa.
Makala
AN-NUUR
8
Na Dr. Noordin Jella
Makala
RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013 pamoja na kwamba hakuna aliyechagua azaliwe na dini gani, nikiwa na maana kwamba wote tumefuata dini walizokuwa nazo wazazi wetu, ingawa kuna wachache ambao wamevuka barabara na kujiunga na dini nyingine kwa sababu za ndoa, uchumi, ushawishi fulani au maamuzi tu ya mtu mwenyewe. Kulingana na uelewa wa viongozi wetu tangu nchi hii ipate uhuru, ni kwamba kila mtawala alijitahidi kuwasogeza maumini wenzie karibu na yeye kadri ilivyowezekana, kwa mfano: Nyerere alipoingia Ikulu kwanza inasemekana aliandika Waraka wa kuwaagiza viongozi wa wizara ya elimu kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa Kikristo, na baada ya kufanya hivyo akahakikisha kwa vitendo kwamba anawapendelea Wakristo kwa kila hali. Hii ni vita kubwa sana, pamoja na kwamba siyo vita ya kutumia bunduki au mapanga lakini ni vita ambayo imeweza kudumu kwa zaidi ya miaka 50 sasa; pamoja na kuwepo kwa vita hii, lakini hakuna kiongozi hata mmoja utakayemuuliza kuhusu vita hii akubali kwamba kuna vita! Kuna msomi mmoja wa Uingereza alikuwa anaitwa Isac Newton ambaye aligundua taratibu za mwendo (principles of motion): moja ya taratibu hizo inasema Kila kitendo kina jibu lake (Every Action has Reaction). Nimetumia taratibu za Newton ili nielezee kwamba Mkiristo akimtoa Muislamu kwa maana ya kwamba ni Muislamu, basi Waislamu wengine walioko ndani ya System hiyo hiyo wanajibu mapigo chini kwa chini; Muislamu akimtoa Mkiristo na kumuweka Muislamu kwa maana za kidini, basi Wakristo waliopo ndani ya System hiyo hiyo wanajibu mapigo ya chini kwa chini. Wewe kama ni Mkiristo, u k a m c h a g u a Wa z i r i Mkristo au wewe kama ni Muislamu ukamchagua Waziri Muislamu bado hujafanya kitu kwa vile waziri si mtendaji bali waziri ni mzungumzaji, lakini wanaopika mambo huko jikoni huwajui kama
Inaendelea Uk. 9
AN-NUUR
SIASA ni mchezo mchafu, na ukitafakari zaidi kuhusu msemo huu, utagundua kwamba wanasiasa ni watu wachafu na hutakiwi kuwaamini hata siku moja. Mwanasiasa yeyote haijalishi anaapa kwa kutumia Quran au Bibilia, madhali ni mwanasiasa hata kiapo chake hakifiki kwa mungu. Wengi wapo kama popo, akifika msikitini ameshika tasbihi, na akiingia kanisani amevaa msalaba! Binadamu ameumbwa na ubinafsi wa kujipendelea, wakati wowote na popote pale alipo hata akipata fursa ya kuamua, basi hatasita kujipendelea. Atajipendelea kwa kuonyesha kwamba yeye ni bora zaidi kuliko wale waliomzunguka. Wakati mwingine anaweza kujipendelea kwa kudhihirisha kwamba imani yake ni bora kuliko imani ya wengine, au mila za kabila lake ni bora kuliko zingine nakadhalika. Imani za udini katika nchi yetu zina historia ndefu mno licha ya kwamba wanasiasa na serikali zao zimekuwa zikikataa kwamba hakuna ubaguzi wa udini katika nchi hii. Kulingana na utafiti wangu hulka za udini pia zimechangia kulinda na kujenga desturi za kulindana: mtu anakosa ambalo kwa mujibu wa sheria anastahili kuwajibishwa kwa kufikishwa mbele ya haki, lakini kwa vile ni muumini mwenzio, basi unamlinda, na huku ukizingatia kigezo kwamba ukimfukuza utapunguza idadi ya waumini katika safu ya uongozi wako. Imeshawahi kutokea mtu amekosa lakini kigezo cha imani za kidini kikamlinda asifukuzwe kazi bali akahamishiwa idara nyingine ili akajirekebishe! Wa k a t i m w i n g i n e udini unatumika kama njia mbadala ya kuugawa umma ushindwe kusimama kwa pamoja kama taifa kutetea mahitaji muhimu na maslahi kwa taifa (Divide and Rule). Taifa hili ni la Waislamu na Wakristo ukiwagawa wakawa hawapendani,
wanagombana na kuchukiana, basi wanakuwa hawana uwezo wowote wa kuukemea utawala wala kuuwajibisha pale wanapoenda kinyume na taratibu zilizowekwa; na kwa maana hii watawala wanaweza kufanya watakavyo wanajua hakuna nguvu ya umma ya pamoja ya kuwawajibisha. Hii katiba tunayoitafuta hivi sasa tungekuwa tumeshaipata miaka mingi iliyopita tangu enzi za Nyerere, lakini tumegawanywa na tumegawanyika. Mwaka 1992 tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi vya kinaki, ni wanasiasa hao hao
waliokuwa serikalini waliokuwa mustari wa mbele katika zoezi hilo la kuviunda vyama vya upinzani, na walipomaliza kuviunda wao hao hao ndiyo walianza kutuambia kwamba hiki ni chama Wa i s l a m u n a k i l e n i chama cha Wakristo au chama fulani ni chama cha kikabila nakadhalika! Ilimradi tu wametugawa na kweli tumegawanyika. Tatizo la Udini ni tatizo sugu na lina historia ndefu katika nchi hii, na tatizo hili hakulianzisha Dr. Kikwete licha ya kwamba watu wengi wanalalamika kwamba Kikwete ana Udini. Udini aliuanzisha Mwalimu Nyerere mwenyewe hata
kabla nchi haijapata uhuru toka kwa Waingereza, na kauli ya kwanza ya Udini aliitoa Nyerere akiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Dar es Salaam aliposema Hapa nipo Mkristo peke yangu wakati akitoa kauli hiyo alikuwa amezungukwa na baadhi ya wanaharakati wa chama cha TAA waliokuwa wanapigania uhuru wa nchi hii ambao wote walikuwa ni Waislamu. Wakati watu wanashauku ni namna gani wanaweza kupata uhuru yeye hakufikiria umuhimu wa uhuru kwanza, bali alikiria Udini! Pamoja na kwamba hakuna anayejua dini nzuri ni ipi? Au
9
Inatoka Uk. 8
Makala
RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 25-31, 2013 alivyokuwa anashangaa! Mimi nikaona labda kwa vile ni walimu wenzangu, labda walikuwa wanafanya utani, lakini cha kushangaza nikaona gumzo hilo likawa refu na baada ya hapo ikawa inaendelea minongono ya chini kwa chini! Na wengine wakaanza kuniita Abdala, wakati hilo siyo jina langu! Je, kama ningekuwa ni Bhudist au sina dini yoyote
AN-NUUR
ni Waislamu au Wakristo!
Hii ni vita ya kipuuzi na inabidi vita hii ikomeshwe mara moja, kwa vile tukiendelea na ustaarabu huu tutajikuta siku moja tunatoana ngeu. Tusihusishe mahitaji muhimu ya binadamu na imani za kiroho. Kila binadamu bila ya kujali imani yake ya kidini anahitaji kula, kunywa, kuvaa, elimu bora na mengineyo. Hivyo kuhusisha imani za kiroho na mahitaji muhimu ya binadamu, ni kumkufuru mungu. Watu wengi wanamlaumu sana Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwamba ni mtu anayeendekeza udini, lakini kwa nini tumlaumu Kikwete tusiilamu CCM na system yake! Si tunasema kwamba Rais ni taasisi, kama hivyo ndivyo sioni kama tutakuwa sahihi kumlaumu Kikwete, mimi nawaombeni hebu mvute kumbukumbu zenu mkumbuke kukua na kuenea kwa Udini tangu nchi hii imepata uhuru mwaka 1961 hadi leo, ingawa nafahamu kwamba Watanzania tuna kumbukumbu dhaifu; hatukumbuki jana wala hatuna habari na kesho, isipokuwa tunaiona leo tu kwa vile ipo mbele ya macho yetu, lakini pamoja na lawama hizo, Kikwete huyo huyo anaonekana vita ya udini imemshinda kwa vile Wakristo wana vyuo vikuu zaidi ya 15 hapa nchini, wakati Waislamu wana Chuo Kikuu kimoja. Waislamu wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuhusu ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kuwapa Wakristo upendeleo, lakini wamekuwa wakipuuzwa kama wanachosema siyo kitu muhimu! System ya Nyerere (serikali ya CCM) imekuwa na tabia ya kupuza sana wananchi wake. Unaweza ukatoa hoja nyeti sana kwa manufaa ya jamii, lakini wakajikausha kwa kukaa kimya kama vile unachokidai hakina maana! Mtu wa kwanza katika serikali kuzungumzia kubaguliwa Waislamu katika elimu alikuwa Professor Kighoma Malima, lakini Mzee Mwinyi hakuchukua hatua zozote wala kukemea kwa vile ubaguzi huo umewekwa na mwenye nchi. Sasa hivi yupo Rais Kikwete na Maalimu Shukuru Kawambwa hawataki kuuweka hadharani
ningewekwa kwenye kundi gani!? Ningekuwa juu ya Ukristo au ningekuwa chini ya Uislamu!? Je, Watanzania bado hamjakubali kwamba Nyerere katupumbaza? Sasa kama Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu anaweza kustaajabu
RAIS Jakaya Kikwete (katikati), Rais mstaafu Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu mstaafu Yusuph Makamba.
ubaguzi huo wala kuukemea. Wanaogopa wakiukemea wanaweza kuwa katika matatizo makubwa, kwa vile mwenye nchi aliacha wosia kwamba anataka kulipa Kanisa A better chance. Mimi naona kwa mwenendo huu tunazidi kuongeza baruti kwenye mbegu ya chuki iliyopandwa na Mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Nyerere. Nyerere amepanda mbegu ya chuki ya udini kati ya Waislamu na Wakristo na kama tusipotumia busara kuingoa mbegu hii kuichoma moto na kuifukia baharini, basi nchi hii siku za usoni itawaka moto! Hivi majuzi Waislamu walilalamika wakidai serikali wamechakachua matokeo yao ya mtihani ya kidato cha Nne/Sita! Hizi ni shutuma nzito sana kwa nchi yoyote inayojali r ai a w ak e n a inayopenda kudumisha amani ya kweli, na shutuma kama hizi si vizuri kutumia ujanja
kwamba kumbe Muislamu anaweza kujua hesabu!? Hivi imani ya kiroho na uelewa au ufahamu wa mtu vinahusiana nini!? Ina maana Professor wa hesabu Mkiristo akibadili dini na kuwa Muislamu hesabu zote kichwani zinayeyuka na kuwa muuza machungwa?
Ndugu zangu Watanzania, Nyerere ametufanya kitu kibaya sana, na kama tusipotumia busara tutakuja kuchinjana kama kuku kwa imani za kijinga ambazo hazitofautiani na imani za kishirikina. Mimi binafsi ni muhanga wa sera za Udini, naamini kwamba sera na vigezo hivi hivi vya udini ndivyo vimetumika kuvipiga vita na kuviagandamiza vitabu vyangu ndani na nje ya nchi. Wanakitengo wakitumia desturi na mila zao zile zile za Udini za kwamba kwa nini Muislamu aandike vitabu vingi kiasi hiki (Vitabu
33)? Vitabu hivi vinaweza kuonekana kwenye mitandao kama vile www. amazon.com, www.google. com, na mingineyo (tafuta Noordin Jella). Udini umeleta chuki za
ujanja wa kuzizima chini kwa chini, bali ni suala ambalo serikali inatakiwa ijisafishe wazi wazi ili kuondoa chuki ambazo zinaendelea kujilimbikiza; na wale wote waliohusika ni lazima wawajibishwe kulingana na mujibu wa sheria. Mwaka 2007 nilipokuwa nafundisha kule Chuo Kikuu Mzumbe siku moja
NAPE Nnauye, Katibu Mwenezi CCM nilikuwa nasahihisha mtihani wa wanafunzi wangu wa mwaka wa tatu ambao nilikuwa nawafundisha somo la Quantitative Economics (Mahesabu ya Uchumi); wakati nasahihisha mtihani huo akauona mwalimu mwenzangu ambaye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi. Mara akaanza kushangaa eti kumbe ninajua hesabu! Akaanza kustaajabu inakuwaje mimi Muislamu ninajua hesabu? Mara akawaita walimu wengine nao wakaanza kushangaa kama yeye
watakipinga.. (Dr. Noordin Jella (Ph. D. in Economics) Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU D a r, U n i v e r s i t i e s . Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political Analyst Email: norjella@yahoo.com Mobile: +255 782 000 131)
kijinga ambazo zimepuuza kabisa kitu kinachoitwa uzalendo. Leo Muislamu amefanya kitu kizuri, Wakristo wanakipinga; kesho Mkiristo naye atafanya kitu kizuri kwa taifa hili lakini Waislamu
10
Makala
AN-NUUR
Balozi wa Marekani nchini Syria kulitangazwa mapema 2010. Mahusiano ya kibalozi yalikuwa yamevunjwa mwaka 2005 baada ya kuuawa kwa (aliyekuwa Waziri Mkuu wa Lebanon) Rak Hariri, ambako Washington iliilaumu Syria kwa mauaji hayo/ Ford aliwasili nchini Syria takriban miezi miwili kabla ya kuanza kwa uasi. Jeshi Huru la Syria (FSA) Washington na washirika wake walirudia nchini Syria vielelezo vikuu vya Mkakati wa Salvador nchini Irak, na kukia kuundwa kwa Jeshi Huru la Syria (FSA) na vikundi vyake tofauti vya uasi ikiwa ni pamoja na kikundi mwanachama wa Al Qaeda cha brigedi za Al Nusra. Wa k a t i k u u n d w a k w a Jeshi Huru la Syria (FSA) kuliotangazwa Juni 2011, kusajili na kutoa mafunzo kwa askari wa kukodiwa kutoka nje kulianzishwa kitambo kabla. Katika maeneo mengi, Jeshi Huru la Syria ni vungavunga tu. Linainuliwa na vyombo vya habari vya Magharibi kama chombo halisi cha kijeshi kilichoundwa kutokana na askari wengi kuyakimbia majeshi ya serikali. Idadi halisi ya waliokimbia jeshi la serikali haikuwa muhimu au ya kutosha kuunda mfumo halisi wa jeshi, wenye mamlaka za utawala na udhibiti. FSA siyo jeshi halisi la watu wa fani hiyo, ila ni mkusanyiko au mtandao wa brigedi tofauti za ugaidi, ambao wanaunganisha pamoja vikundi vya kijeshi vinavyojitegemea, vikifanya opereseni sehemu tofauti za nchi. Kila moja kati ya vikundi hivi vya kigaidi inafanya kazi kivyake. FSA haina mfumo mmoja wa kutoa amri na kudhibiti kinachotokea, na kuwasiliana na vikundi tofauti vya kijeshi. Vikundi hivi vinaelekezwa na vikosi maalum na mawakala wa usalama wa Marekani na NATO ambao wamepachikwa katika mifumo ya vikundi kadhaa husika. Vikosi hivi maalum (vyenye mafunzo ya hali ya juu) katika mapigano (wengi wao ni waajiriwa wamakampuni binafsi ya ulinzi) wanawasiliana kila mara na vituo vya upelelezi wa kijeshi vya Marekani na washirika wake wa NATO, pamoja na Uturuki. Vinaelekezwa na vikosi maalum (vikiwemo SAS ya Uingereza na askari wa miavuli wa Ufaransa) na makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yenye mikataba na NATO na makao makuu ya Jeshi la Marekani (Pentagon). Kwa hili, taarifa zinathibitisha kukamatwa na serikali ya Syria kwa waajiriwa 200 hadi 300 wa makampuni binafsi ya ulinzi ambao walikuwa katika vikundi vya uasi. (itaendelea)
Mapinduzi ya Kiislamu nchini Irak (SCIRI), kuwa wanahusika na mauaji hayo. Pia waliituhumu Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuendesha ugaidi wa dola (kwa mujibu wa Financial Times, gazeti mashuhuri la Uingereza). Makomandoo wa polisi pamoja na Brigedi ya Mbwamwitu walikuwa wanasimamiwa na mpango wa kupambana na ugaidi wa Marekani, katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Irak. Makomandoo wa polisi waliundwa chini ya uangalizi wenye uzoefu na wapiganaji dhidi ya ugaidi wa Marekani, na kuanzia mwanzo walifanya operesheni za pamoja na vikosi maalum na vya siri vya jeshi la Marekani, kwa mujibu wa taarifa za usalama wa taifa la shirika la habari la Reuters. Mshirika muhimu katika kukua kwa Makomandoo Maalum wa Polisi alikuwa James Steele, mshirika wa zamani wa vikosi maalum vya Jeshi la Marekani ambaye alionja vita huko Vietnam kabla ya kuendelea mbele, kusimamia ujumbe wa kijeshi wa Marekani nchini El Salvador wakati wa kilele cha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo..... Mchangiaji mwingine wa Marekani alikuwa yule yule Steven Casteel ambaye, alikuwa osa mwandamizi zaidi mshauri katika Wizara ya Mambo ya Ndani alipuuzia taarifa zenye ushahidi kamili wa uvunjwaji usio na mipaka wa haki za binadamu kama uvumi na vijembe. Kama Steele, Casteel alipata uzoefu katika Amerika ya Kusini, kwa upande wake akishiriki katika kumtafuta
maporini mbabe wa madawa ya kulevya Pablo Escobar katika vita dhidi ya madawa nchini Colombia miaka ya 1990...... Alichofanya Casteel huko nyuma ni muhimu kwa sababu aina hii ya kukusanya taarifa za kijasusi na kutayarisha orodha za watu wa kuuawa ni sehemu mahsusi ya kile Marekani inachofanya inaposhiriki katika programu za kupambana na ugaidi na kunadhihirisha uwiano wa kile kilichotokea na kuonekana kana kwamba ni mauaji ya mtawanyiko, yanayotokea ghaa tu. Mauaji haya ya halaiki yanayoratibiwa rasmi yanaendana na kile kinachotokea Irak, Pia yanaendana na kile kinachofahamika kuhusu Makomandoo wa Polisi Maalum, ambayo ilifukwa kuipa Wizara ya Mambo ya Ndani uwezo wa kutumia vikodi maalum vya wapiganaji (kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani). Ili kuendana na nafasi hiyo, makao makuu ya Makomandoo wa Polisi yamekuwa ndiyo kitu cha kamandi maalum ya kitaifa, udhibiti, mawasiliano, kituo cha uendeshaji kumpyuta na ujasusi, kwa usimamizi wa Marekani (kwa mujibu wa Max Fuller, aliyetajwa juu). Maandalizi ya mwanzo yaliyofanywa chini ya Negroponte mwaka 2005 yalitekelezwa chini ya mrithi wake, Balozi Zalmay Khalilzad. Robert Stephen Ford alihakikisha uendelezaji wa mradi huo kabla ya kuhamishwa kuwa Balozi wa Marekani nchini Algeria mwaka 2006, na pia aliporudi Baghdad kama naibu balozi, mwaka 2008. Operesheni Contra wa
11
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Kuna kijana mmoja aliwahi kuishi katika nchi hii, na huyu kijana alikuwa anaitwa Edward Moringe Sokoine. Kijana huyu alikuwa anatoka kabila la Wamasai. Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hii na alipokuwa Waziri Mkuu alikuwa mtu wa kwanza kumrekebisha Nyerere hadharani kwa kusema Tusiseme Zidumu Fikira za Mwenyekinti wa CCM, Bali Tuseme Zidumu Fikira Njema za Mwenyekiti wa CCM; Ujasiri huu ulikuwa siyo wa kawaida, ilikuwa si rahisi kwa mtu yeyote kumkosoa Nyerere, Nyerere alikuwa hakosolewi, harekebishwi na wala hashauriki, alikuwa Mungu Mtu! Sokoine alipokuwa Waziri Mkuu alianzisha kampeni ya kupambana na Wahujumu Uchumi kwa wakati huo au kwa sasa tunawaita Mafisadi, Sokoine aliwahi kuwapa baadhi ya vigogo wa serikali siku saba warudishe pesa za wananchi shilling million sitini (Tsh. 60,000,000) za wakati huo ambapo dollar moja ya Kimarekani ilikuwa Shillingi 20. Vigogo hao walidaiwa kumuuzia Lord Rajipar Meli ya serikali na pesa hazikuonekana. Basi Sokoine katika kampeni zake za kupambana na Ufisadi akawapa siku saba kwa kuwaambia kuwa anawapa Siku Saba warudishe Pesa za Wananchi, la wakishindwa atawapeleka Radio Tanzania wakawaambie Watanzania kwa Njia ya Radio Pesa Zao wamezipeleka Wapi?; Mimi Naenda Dodoma Kuhutubia Bunge, Nikirudi Nipate Majibu. Kwa bahati mbaya kabla ya siku saba kutimia Sokoine alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea huko Dakawa Morogoro akitokea Bungeni Dodoma. Watanzania wenzangu kama mmeyasahau haya naomba mtafute kumbukumbu kwenye maktaba za Radio Tanzania na Magazeti ya Tanzania wakati huo (Uhuru,
Mzalendo, Daily News & Sunday News); nakumbuka yalitangazwa kwenye taarifa ya habari wakati huo na kwenye magazeti yote yaliandika. Sokoine alipofariki ndipo harakati za kupambana na Usadi za kweli zilipoishia hapo na kuzikwa rasmi nje kidogo ya mji wa Morogoro kando ya njia ya kwenda Dodoma, na baada ya hapo yakaendelea maneno yale yale ya majukwaani tu ya kulaani na kukemea rushwa na usadi bila ya vitendo! Je, wale wakubwa wenzangu waliokula chumvi nyingi kama mimi, haya wanayakumbuka, au yakitokea haya walikuwepo Ughaibuni!? Ina maana Nyerere alikuwa hajui kwamba Kawawa ameuza meli ya Wananchi kwa Shillingi million sitini? Wakati nchi ilikuwa na meli moja tu! Sasa wale wanaosema angekuwepo Nyerere haya yanayotokea yasingetokea, naomba waseme au wajibu hoja hii. Leo hii tunashangaa ufisadi wa kawaida unaofanywa na baadhi ya mawaziri na viongozi wa umma. Sokoine alipofariki ufisadi huo wa kutisha
ukaisha kimya kimya hakuna aliyejitokeza kuhoji swala hilo tena! Ndugu zangu Watanzania kabla hatujafikiri kesho kutakuwaje, lazima tukumbuke jana kulikuwa vipi. Huwezi kufanya utabiri wa hali ya uchumi (economical prognosis) wa mwaka kesho kama huna takwimu za mwaka jana. Ukitaka kufanya utafiti wa jambo lolote lile, ni lazima kwanza uelewe kitu kinachoitwa Chanzo cha Tatizo au kwa jina la Kiingereza Background of Problem. Bila kujua chanzo cha tatizo la Usadi la nchi hii, hata tufanye nini au hata tumpate nani, au kitawale chama gani, hatutaweza kumaliza usadi. Rais Mwinyi aliukuta usadi, akauacha na Rais Mkapa naye akaukuta na kuendeleza yale waliofanya watangulizi wake kwa vile Katiba ni ile ile na watu ni wale wale. Rais Kikwete naye hawezi kumaliza Ufisadi hata tungelala barabarani mwaka mzima, hawezi kubadilisha chochote kwa vile yeye ni mzungumzaji tu lakini System anayoisimamia ni System ile ile ya Nyerere na chama chake kile kile
cha CCM. Enzi za Nyerere pamoja na Tanzania kuwa na wasomi wengi waliokuwa wamefika vyuo vikuu, lakini katika uchaguzi mkuu wa Urais, Nyerere alikuwa anagombea na Kivuli yaani kwamba hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kugombea nafasi ya Urais na yeye, na chini ya picha yake kulikuwa na neno Ndiyo na chini ya kivuli kulikuwa na neno Hapana. Hivyo ukichagua neno ndiyo Umemchagua Nyerere, na ukichagua neno hapana pia Umemchagua Nyerere! Huyo ndiye Nyerere niliyekuwa ninamjua mimi. Jambo la kushangaza ni kwamba katika nafasi za Ubunge walikuwepo wagombea wawili wawili wakiwakilishwa na alama ya Jembe na Nyumba. Nakumbuka Nyerere watu walikuwa wanamtania wanamwita Haambiliki yaani Nyerere ni mtu aliyekuwa hapendi ushauri wa mtu yeyote yule. Wanaomjua Nyerere vizuri wanasema huwezi kumkalisha chini umshauri, hatakusikiliza, ukitaka atumie ushauri
Inapenda kutoa shukran zake za Dhati kwa mahujaji wote waliosari na Ahlul-daawa. Pia inatangaza kua imeandaa safari ya Umra Mfungo wa Saba ni sawa na machi 11 2013 kwa Gharama ya Dola 1450 tu. Inaendelea kuandikisha mahujaji kwa Mwaka 2013. Wale watakao jiandikisha na kufanya malipo mapema watapata punguzo maalumu la bei. Usisahau Ahlu Daawa Hajj kwa Bei nafuu na huduma bora. Kwa mawsiliano piga simu zifuatazo. Dar es salaam: 0773 724444, 0715 786101 na kwa Zanzibar 0777 417736, 0777484982.
AHLU-DAAWA HAJJ
wako unatakiwa aidha uandike uache wazi aje asome bila wewe kuwepo, au uwepo chumba cha pili uongee kwa nguvu asikie lakini usijue kama anakusikiliza. Nyerere aliwahi kwenda Marekani kuomba msaada wa chakula wakati wa Rais Ronald Reagan, Rais huyo wa Marekani alimshangaa kwa nini apate shida ya kuomba chakula wakati Tanzania ni nchi yenye rutuba na mito mingi. Nyerere alidai hana wataalam wazuri wa Uchumi. Reagan alimshauri kwamba ampe wakulima watano (5) wa Kimarekani waje walime chakula cha kuwatosha Watanzania wote na kingine wauze nchi za nje. Nyerere alikataa akasema yeye ni Mjamaa hataki Mabepari. (Makala hii i m e a n d i k w a n a D r. Noordin Jella (Ph.D. in Economics) Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU D a r, U n i v e r s i t i e s . Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political AnalystEmail: n orjella@ yah oo.com Mobile: +255 782 000 131)
12
Moyoni na dukuduku, na wa dili si wa dini, Wendao huko na huku, na vilembavyo vichwani, Kipyora kizumbukuku, dhidi ya WANAZUONI, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ?
Barua/Shairi
AN-NUUR
MASHEIKH AU WAPOTOSHAJI ?
Nahitaji mbayana, anieleze kiini, Cha wao kuwatukana, MAULAMAA wa DINI, Walounena BAYANA, UKWELI wa QUR-ANI, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Wakajitoa MUHANGA, na kutupwa GEREZANI, Si kwa kusaka FARANGA, bali RADHI za MANANI, MASHEIKH wa kubananga, LENGOLO hasa ni nini, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Wamponda ALBANNA, MWANAZUONI makini, Harakatize mwanana, asozifahamu nani, Watueleze bayana, walofanya wao nini, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Kadhalika MAUDUDI, WAMRADDI hadharani, Mithili ya MURTADI, hali ni MWENZA safuni, Kubwa kwao ni KURADDI, WENZA wao WAUMINI, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Waaidha na QUTUBI, MUHANGA wa GEREZANI, Kwa ya DINI yake HUBBI, akanyongwa KITANZINI, Kwazo zao TAASUBI, WAMKUFURISHA DINI Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? Wawaita MAJAHILI, eti WASOJUA DINI, Si NAHARIi si LAILI, tena KADAMNASINI, Kama hawa MAJAHILI, WAO tuwaite NANI, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAPOTOSHAJI ? TAF-HIMU QUR-ANI, ni TAFSIRI ya NANI, FI-DHWILALI QUR-ANI, MFASIRI wake NANI, Kama si WAO ni NANI, WAPONDAJI NIJUZENI, Hivi hawa ni MASHEIKH, au ni WAKENGEUSHI ? ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.
Written by Stonetown (Kiongozi) // 19/01/2013 // Makala/Tahariri // 5 Comments R I WAYA y a S h a m b a la wanyama (1945), ni moja kati ya kazi nzuri kabisa za kibunifu katika Tasnia ya fasihi andishi hapa duniani. Riwaya hii ambayo iliandikwa na Muingereza ambaye ni maarufu kwa jina la George Orwell, ni mtiririko wa sitiari (allegory) unaoakisi dhana nzima ya ujamaa wa kidemoskrasia katika tawala mbali mbali za kidunia. Kazi hii yenye ubora, ladha na mvuto usiochosha, inahusu kisa cha dola la wanyama. Wanyama ambao kwa pamoja walikubaliana kuungana na kuishi kwa misingi ya usawa na haki. Moja kati ya kanuni hizo za usawa, ilikubaliwa kwamba hakuna mnyama mmoja atakemdhuru mnyama mwengine ama kwa kumla, kumpiga, kumdhulumu na hata kumuuwa. Kanuni hii ilipita na ikaandikiwa kauli mbiu (slogan) isemayo Wanyama wote ni sawa! Kwa muda baada ya kanuni hii kupitishwa na kukubaliwa na wanyama wote, wanyama wadogo wadogo na wale waliokuwa waathirika wa vitimbi, viteweji na mateso ya wanyama wakubwa, walihisi kupata faraja kubwa kwa kuhakikishiwa usalama wao. Imani yao hii ilichangiwa na kuona kauli ile mbiu ikiimbwa na kuandikwa kila kona ya dola lao lile kiasi ya kumfanya kila mnyama
aamini kile anachokiona katika kauli mbiu ile. Wa s w a h i l i h u s e m a Taa haachi mwiba wake. Haikutimia wiki, kuna baadhi ya wanyama hasa ndege, walianza kuona dalili mbaya katika jamii yao. Moja ya dalili hio ni kupotea kwa baadhi ya wanyama katika mazingira ya kutatanisha. Kwa lugha nyepesi, kuna baadhi ya wanyama walianza kuwala wengine kimya kimya kila siku. Wa n y a m a w a d o g o walipogundua usaliti huu walirudi kwa mkubwa wao kushitaki na kusimulia masikitiko yao juu ya kitendo hiki cha uvunjifu wa amani, na usalama wa wanyama katika dola yao. Kwa bahati mbaya walipoka mahala pa mashtaka na kueleza makosa yao, waliona ile kauli mbiu imebadilishwa kidogo kutoka ilivyokuwa mwanzo. Awali kauli ilisomeka Wanyama wote ni sawa, lakini sasa inasomeka Wanyama wote ni sawa, lakini baaadhi ya wanyama, ni sawa zaidi kuliko wengine! Kisa hichi kikaishia hapo. Kumalizika kwa kisa hiki ndipo tunapopata nadharia hiyo niliyoitumia katika kichwa cha makala hii hapo juu, ambayo ni moja ya nadharia maarufu duniani kwa sasa. Yaani nadharia ya Ki-Orwelli. Nimewajibikiwa na kuandika kwa kusema kuwa kwa namna mchakato mzima wa maoni ya katiba unavyokwenda, nanusa harufu ile ile waliyoinusa wanyama wadogo kama mimi katika Shamba la
wanyama. Harufu ya kwamba kuna baadhi ya wanyama ni sawa kuliko wengine. Na hii si tuhuma kutoka katika ombwe la uwazi, bali ina kila aina ya ithibati na visherehesho vya kuutilia shaka mapema mchakato huu wa katiba nchini. Nilitegemea iwapo maoni ya katiba yalilenga kukusanya maoni ya wananchi, kwa haki na usawa, na ili yanipe imani kuwa haki itatendeka, basi yalikuwa yafanywe kwa wanachi wote bila kuweka tabaka (strata/ social classes). Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika mchakato wa katiba, wananchi wote, wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo, viongozi na waongozwa, mashehe na mapadiri, wanasiasa na majeshi, wote kwa pamoja ni wananchi walio sawa. Na mchakato wa katiba ulikuwa uanze na kauli mbiu hiyo ya Wananchi wote ni sawa mbele ya haki na sheria! Kuwe na usawa kwamba, maoni ya katiba yafanyike kama vile tunavyofanya uchaguzi. Yapitie kimajimbo au maeneo ya ukazi wa wananchi. Sasa maoni yakifika jimbo ambalo kiongozi mkuu wa nchi au mstaafu anapoishi, basi hio ndio iwe zamu yake ya kwenda kutoa maoni hapo kwao. Kwa mfano, ikiwa Rais wa Zanzibar anaishi Mbweni, basi maoni yakika jimbo la eneo hilo, iwe ndio zamu yake ya kutoa maoni na wananchi sawia, ijapokuwa atapewa nafasi ya kwanza kufanya hivyo, Inaendelea Uk. 14
13
Makala
AN-NUUR
Alhamdulillahi Wahdahu Lasharikalahu, waswalatu wasalamu ala Nabiyina Muhamad (S.A.W), amma baadau Mheshimiwa Mufti, mtoto wa jongoo alipotaka kutembea alimuuliza mama yake aende vipi? Atangulize mguu upi mwanzo, lakini jibu alilolipata kwa mama yake ni kumwambia nenda mwanangu nenda. Mheshimiwa Mufti na Waheshimiwa wazee wetu na masheikh wetu, na mimi nimewekwa katika mtihani huo huo. Sioni haja ya kutoa hotuba ya uzinduzi wa Baraza la Ulamaa mbele ya visima vya elimu ya dini yetu. Chochote nitachokisema basi si zaidi ya tone moja la chumvi ndani ya bahari ya elimu yetu ya dini. Naomba kwa Uradhi wenu mniruhusu niseme machache ambayo yatakuwa na kasoro nyingi mbele ya wazee mliobobea katika misingi ya dini. Nawaombeni radhi sana kwa hayo. HISTORIA YA ZANZIBAR NA UISLAM Mapema tu, mnamo karne za nyuma watu wa kale kama vile Sumerians, Assyrians, Hindus, Egyptians na Waarabu wa Kusini walitembelea mwambao wa Afrika ya Mashariki ambapo walikutana na makabila ya kienyeji kama vile Wahadimu, Wapemba na Watumbatu. Waarabu hawa, hasa kutoka Ghuba ya Uajemi (Persion Gulf) ndio walioanza kuuleta Uislamu na Wazanzibari wakaikubali kwa dhati dini hii. Wa n a h i s t o r i a w e n g i wanaamini kuwa Uislamu umeingia mapema kabisa katika mwambao wa Afrika y a M a s h a r i k i . Wa k a t i mwanahistoria maarufu wa Moroko Ibun Battuta alipotembelea eneo hili alikuta wakazi wake ni Waislamu na Kiarabu ndio lugha ya fasihi kwa biashara. Mnamo mwaka 1503 Zanzibar ilikaliwa na Wareno lakini katika karne ya 17 kulikuwa na ghasia katika mwambao huu ikiwemo Pemba. Mwaka 1652 Waarabu waliivamia Zanzibar na waliiteka Mombasa, Pemba na Kilwa mnamo mwaka 1698 na
wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri na wakausiana kufuata haki na wakausiana kushikamana na subira (yaani) kustahamiliana. Jukumu hili nalo ni kubwa na ni zito lakini ndio wajibu wetu, na ni lazima kulifanya. Tukilifanya kwa misingi tuliyoielezea hapo juu basi nasi tutakuwa katika kundi la wataokuwa na kheri, Inshaalla Mwenyezi Mungu atujaalie kila la kheri, na kulitekeleza jukumu hilo zito kwa njia ile anayoipenda Mwenyezi Mungu. Ammin. MABADILIKO YA TABIA YA BAADHI YA WAUMINI Mheshimiwa Mufti, Waheshimiwa Maulamaa visiwa vyetu hivi vimekumbwa na wimbi kubwa la mabadiliko ya baadhi ya waumin. Ni ukweli usiopingika kuwa wakati wetu umekuwa na wasemaji wengi sana wanaozungumzia mambo ya kiislamu tokea mambo ya USULI hadi ya FURUU mambo haya yote yanahitaji elimu ya kina na hekimu kubwa hali ya kuwa wao sio Ahli wa ilmu. Bahati mbaya kila msemaji hupata wasikilizaji, mashabiki na hata waenezaji na wenye kuyanusuru maneno hayo. Hali hii imeleta mtafaruki mkubwa baina yetu, ikazaa migongano na hatimae makundi yenye kupingana ambayo yameidhoofisha dini na jamii yetu. Ni kweli Uislamu haukuweka tabaka la watu wadini na wasio wa dini, lakini pia haukuwacha mambo shaghala baghala. Mtume Muhammad (S.A.W) amesema wanachuoni ndio warithi wa Mitume. Tunajua kuwa umoja wetu wa Kiislam na mshikamano wetu wa sasa unaaza kumongonyoka. Kwa maana hiyo tujitahidini kufuata na kuhimizana maagizo ya Qur-ani:Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote kwa pamoja na wala musifarikiane Hata katika hadithi tunatanabahishwa kwamba Hakika mfano wa Waislamu katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kurehemeana kwao ni sawa sawa na kiwiliwili kimoja Ni wajibu wenu mlio hapa, kuyajadili mambo kama haya Inaendelea Uk. 14
MUFT wa Zanzibar majina yasiyopungua sita (6) kwake kwa kutolewa fat-wa kutoka kwa Mufti. na kufanya kazi nyengine iii. Naibu Mufti, Kadhi litakazopewa na Mufti. Mkuu, Naibu Kadhi Mkuu, Kazi zenu ni ngumu na Katibu Mtendaji Kamisheni zinahitaji uadilifu mkubwa, ya Wakfu na Mali ya Amana kujitolea, haki na ukweli. na Mwalim Mkuu Chuo cha Ndio maana Imamu Ibnu Kiislam ambao wao wanaingia Qaym amewaita wanachuoni kutokana na wadhifa wao. kuwa ni watia saini (signatory) Makatibu wa vikao hivi kwa niaba ya Mwenyezi watakuwa Katibu wa Mufti Mungu. Sina wasi wasi hata na Msaidizi wa Katibu chembe wa mambo haya wa Mufti. Baraza hili kwa juu yetu. Naamini na sote mujibu wa kanuni ya 5 tunakubali kuwa Baraza linatakiwa likutane angalau limepata wajumbe wenye mara mbili kwa mwaka na elimu, busara na hekma, wanaweza kufanya kikao cha waadilifu na wakweli; na dharura pale inapohitajika. hivyo basi msingi mkubwa Mufti chini ya kanuni ya wa mafanikio wa kazi zenu na 5(2) anaweza kuunda kamati wajibu wenu tunao. Haya sote maalum itayoshughulikia tunayaelewa pale Mwenyezi tatizo lililojitokeza ila ni Mungu alipotutanabahisha lazima atilie maanani suala katika Suratul Al-Ahzab zima la uwakilishi katika kamati hiyo, na kwamba kwa kutukumbusha kuwa maamuzi ya kamati hiyo tutawakal kwa Mwenyezi y a n a w e z a k u k u b a l i w a , Mungu na Mwenyezi Mungu kutenguliwa au kufanyiwa anatosha kuwa mlinzi na kuwa marekebisho fulani katika sote tulioamini tumuogopeni kikao cha Baraza zima la Mwenyezi Mungu na tuseme maneno ya kweli. Maulamaa. Tunapoyafanya hayo kwa uadilifu, ukweli na haki kama KAZI ZENU Wazee wetu, Masheikh ilivyo kawaida yenu, na na Maulamaa wetu, wajibu tukavuta subra katika mitihani wenu na kazi zenu zipo chini ambayo tutaipata wakati wa ya kanuni ya 7 ya Kanuni za kutekeleza majukumu haya; Baraza la Ulamaa ambayo basi Mwenyezi Mungu atazidi kuwa nasi. Mwenyezi Mungu inasema: K a z i y a B a r a z a n i mwenyewe anatukumbusha kumshauri Mufti juu ya katika Qur-ani yake, katika Suratul Asr kuwa Binaadamu masuala ya Kiislam yaliyowasilishwa yuko katika hasara isipokuwa
14
Inatoka Uk. 13 na mengine zaidi ya haya ili mumshauri Mufti ipasavyo. Kamba hii ya Mwenyezi Mungu ambayo sasa waislam wanaanza kuihujumu inahitaji kulindwa isikatwe katwe. Nyinyi Baraza la Ulamaa ndio walinzi wetu. Roho zetu, macho, nafsi tamaa na kiu ya waislam wema zinawatazama nyinyi. Naamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtafanikiwa kuielezea dini yetu kwa njia ya fat-wa na njia nyingi nyenginezo kwa kuielemisha jamii, kwa maslahi yetu na kizazi chetu na dini yetu. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuwa kuna vyuo (maahad) vingi vinavyotoa elimu bora na vyuo hivyo vina walimu wazuri Unguja na Pemba. Hata hivyo kwa kukosekana umoja wa vyuo hivyo imekuwa tabu kwa mwanafunzi anaemaliza thanawi kujiunga na vyuo vikuu vyetu pamoja na kuwa vyuo vya nje wanakubaliwa. Natumai mtamshauri Mufti ili tuone namna gani tutaunganisha maahad zetu na kuwawezesha wanafunzi wake kunufaika na vyuo vikuu vyetu katika fani zao. Sadaka hazianzi nje bali kuanzia nyumbani. UHURU WA DINI /KUABUDU NA HAKI ZA MTU Bila shaka Uislamu ni dini iliyotoa uhuru mkubwa kwa mwanaadamu kiasi cha Allah kukataza watu kulazimishwa kufuata dini. Uhuru ndio unaomtofautisha mwanadamu na malaika. Hata hivyo uhuru huo umeambatana na majukumu kwani hakuna uhuru usio na mipaka. Kikawaida Uislamu unaangalia zaidi dhima (majukumu kuliko uhuru). Amesema Mtukufu, Subhanahu Wataala kuwa (na naapa) kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila shaka amefaulu aliyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amehasirika aliyeiviza (Suratu Ash-Shams aya 7-10). Ili kujenga utawala wa sheria, haki na kulinda amani na utulivu nchi yetu inaamini dhana ya uhuru na haki za binadaamu. Kwa tafsiri iliyo rahisi ni kweli kifungu cha 18(1) na (2) cha Katiba kinachotowa uhuru wa maoni, kifungu cha 19(1), (2) na (3) kuhusu uhuru wa mtu kuamini dini atakayo na kifungu cha 20(1) kuhusu uhuru w a k u j i k u s a n y a , vinaruhusu watu au waumini kufanya wanayotaka kwa kisingizio cha Katiba yetu ya Zanzibar. Ni kweli vifungu vyote hivyo vinatoa uhuru wa muumini yeyote kufanya kile anachohisi ndani ya maoni yake. Lakini muumin huyo huyo anatakiwa asisome baadhi ya vifungu tu kwa maslahi yake, lakini avisome vifungu vyote vinavyohusiana na maudhui inayohusika. Sasa, kwa maana hiyo ukisoma vifungu vya Katiba vya 18, 19 na 20 ni lazima usome kwa pamoja na kifungu cha 23(1), (2), (3) na (4) pamoja na kifungu cha 24(1) kama vinavyojielezea hapo chini: 23(1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na Sheria za Zanzibar, kuchukua hatua za kisheria kama zilivyowekwa, kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi. (2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuheshimu mali ya mtu mwengine. (3) Watu wote watatakiwa na sheria kulinda vizuri mali ya Zanzibar na kwa pamoja kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa Zanzibar kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadae ya Taifa lao. (4) Kila Mzanzibari ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi, kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa Zanzibar. 24(1) Haki na Uhuru wa binadamu ambayo misingi yake imeorodheshwa na Katiba hii haitatumiwa na mtu mmoja kwa namna ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma na inaweza kubanwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi iwapo tu kibano hicho ni lazima na kinakubalika katika mfumo wa kidemokrasia.. Masheikh wetu, misingi hii ya Katiba naamini itawasaidia sana katika kazi zenu ambapo baadhi ya waumini hutumia vibaya uhuru wao na kusababisha fujo, kuingilia mali ya umma na kadhalika. Hivi sivyo na ni wajibu wetu sote na zaidi Baraza lenu tukufu kuwaelimisha sana waumini wa aina hii misingi mizuri ya dini, silka, tabia na khulka zetu za kiislam ambazo siku zote zinataka
Makala
AN-NUUR
wananchi wote wa Zanzibar, yanawezajae kuyapindua maoni aliyoyatoa Mkapa na Mwinyi? Sipati picha! Yaani, hivi kweli maoni ya wananchi wa kawaida yatasikilizwa bora kwa kulinganisha wingi wao kuliko ukubwa na maoni ya wenye cheo, kauli, na nguvu katika nchi hii? Hili si kweli, maana tumeona katika chaguzi nyingi hapa nchini, ambapo sauti ya wananchi walio wengi ikipinduliwa na kauli ya mtu mmoja. Hili liko wazi kama sabuni ya mche! Na ndio hapa ninapoona kuwa ile kauli mbiu isemayo Watu wote ni sawa mbele ya haki na Sheria ikibadilika na kusomeka Watu wote ni sawa mbele ya haki na sheria, lakini baadhi ya watu, ni sawa zaidi kuliko wengine. Kwa hali hii naanza kukosa imani na kutawaliwa na ruwaza za nadharia ya Ki-Orwell ninapautazama mchakato mzima wa katiba hapa nchini unavyokwenda. Natoa hoja.
15
Makala
AN-NUUR
kuvunja ndoa na kuharibu familia. Makka ilikuwa imepakana na himaya mbili kubwa, Wafursi na Warumi, kwa hiyo Maqurayshi walijaribu kusisitiza kwamba Muhammad alikuwa akifundishwa Quran na kijana mmoja wa Kikristo aliyeitwa Jabr. Habari hizi zilisambaa sana na hatimaye zikajibiwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe: Na bila shaka tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anayemfundisha (Lakini lugha ya yule wanayemuelekezea (kuwa anamfundisha Mtume) ni ya kigeni na, hii lugha inayotumika katika Quran) ni lugha ya Kiarabu bulbul Qur(15:103). Kufuatia hoja hiyo ya Mwenyezi Mungu, wakuu wa Makka wakatangaza kwamba Muhammad si mtu wa Makka - maneno anayosema yanatoka vyanzo vingine na yeye ameshikamana zaidi na vyanzo hivyo kuliko alivyoshikamana na utamaduni wake, lugha yake ya asili na dini ya mababu zake. Lakini pamoja na yote hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu hakufikiria hata mara moja kubadili kitovu cha Uislamu kutoka Makka kuelekea sehemu nyingine. Maqurayshi, ambao ndiyo waliodhibiti madaraka mjini Makka, hawakukata tamaa kumfukuza Muhammad (saw) kutoka Makka, ikiwa ni pamoja na kupambana naye kwa njia zote. Hatimaye wakaamua kumuwekea vikwazo yeye na ukoo wake. Wakuu wa Makka walikubaliana kumtenga Muhammad (saw) na ukoo wa Bani Hashim na Bani Abdul Mutallib. Hii maana yake hakuna aliyeruhusiwa kufanya nao biashara wala kuoleana nao. Na hati maalumu ya kuwatenga ikabandikwa kwenye Kaabah. Maqurayshi na washirika wao walidhani kwamba hatua hii ya kumtenga Muhammad na jamaa zake kutoka katika
maisha ya Makka kungeleta tija zaidi kuliko mikakati yao ya awali. Hali hii iliendelea kwa takriban miaka miwili au mitatu hivi. Maqurayshi walitarajia kwamba watu wa ukoo wa Mtume wangeanza kumkacha Muhammad (saw), na hata baadhi ya Waislamu wangeachana na Uislamu. Mwisho wake, Muhammad angebaki mpweke, aliyetengwa na jamii na asiyepata msaada wowote. Licha ya yote hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu hakusalimu amri. Bado hakukiria kukimbia na kuhamisha kiti cha Uislamu kutoka Makka kwenda kwenye ngome nyingine. Badala yake, aliibuka kutoka kwenye changamoto hizo na dhamira kubwa zaidi ya kuikomboa Makka. Habari hizi za Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu wake kutengwa kiuchumi na kijamii zikaenea eneo zima la Arabuni. Na watu wenye akili timamu wakaanza kutambua kwamba kuna jambo si la kawaida kuhusu huyu mtu Muhammad. Vipi Mtume wa Mwenyezi Mungu na wafuasi wake na watu wa ukoo wake waliweza kuhimili kutengwa kule? Walikimbilia eneo moja pembezoni mwa Makka, ambapo waliteseka sana na maumivu ya kukosa chakula na mahitaji mengine muhimu. Kuna wakati walikosa kabisa chakula. Waislamu hawa hawakuruhisiwa hata kuzungumza na watu wengine. Ruhusa pekee waliokuwa nayo ni miezi mitukufu ya (al -Ashhur al-Hurum), ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu angeenda Kaaba na kuwaeleza Waarabu wanaotoka nje ya Makka maana ya Uislamu. Vikwazo hivi dhidi ya Mtume na watu wake vikaleta huruma kutoka kwa watu wengine wa Arabia. Wengine walimsikiliza
na wakaitikia vizuri wito wake. Wengine walimpelekea chakula na maji kwa siri. Hali hii iliendelea kwa takriban miaka mitatu, ndipo vijana watano wa Makka walipoibuka na kutamka hadharani kwamba vikwazo hivi ni upotofu mkubwa. Vijana hawa walitafuta namna ya kuondoa lile tangazo lililowekwa kwenye Kaaba. Siku hiyo, mmoja wao akaenda kwenye Kaaba na kuwahutubia watu akisema: Oh Watu wa Makka! Tunakula na kusaza na tunavaa, wakati Bani Hashim wanaangamia bondeni pembezoni mwa Makka, hawawezi kununua wala kuuza! Sitatulia mpaka tangazo lile la kuwatenga kwenye Kaaba lichanwe. Aliposikia hivi, Abu Jahl akajibu kwa sauti: Wewe ni muongo! Na kwa hakika tangazo lille halitachanwa! Kisha kijana wengine wanne wakasogea mbele kuunga mkono kile kilichosemwa na mwenzao. Abu Jahl akatambua kwamba vijana hawa watano walikuwa wakiwakilisha kundi kubwa la watu pale Makka. Kupambana nao kungeleta matatizo makubwa Makka. Kwa hiyo, tangazo lile likashushwa na kuchaniliwa mbali, na Mtume wa Mwenyezi Mungu na watu wake wakaruhusiwa kurejea Makka. Tangu pale, Maqurayshi wakatambua kwamba hakuna kitu kitakachoweza kumzuia Muhammad (saw) kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kufanya kile ambacho Allah (sw) anataka kwenye ardhi. Kipengele cha ushujaa katika Sira ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, kupitia matukio kama haya katika maisha yake, hakizingatiwi kabisa na wale wanaopanga harakati za Kiislamu leo. Wanadhani akili
na uoni wao pekee vinatosha! Inawezekana vipi watu hawaoni jinsi maamuzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu yalivyokuwa imara na yenye kufuata kanuni kule Makka? Ni kweli, kulikuwa na majaribio mawili ya kutafuta msaada au ukimbizi nje ya Makka, Habashah na Ta if. Lakini majaribio haya ya kupunguza madhila ya Waislamu wa awali Makka, hayakuwa mbadala wa kuikomboa Makka. Ushahidi wa hilo ni kwamba, wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoasisi dola ya Kiislamu Madina, bado alielekeza nguvu zake katika kuikomboa Makka. Katika miaka yake kumi Madina, Mtume aliandaa jeshi kubwa, yeye mwenyewe akishiriki mapigano, akapambana vita ya kuikamata Makka na Kaaba, ili ziwe ngome ya Mamlaka ya Kiislamu. Wapi pengine, wakati Mwenyezi Mungu mwenyewe ameshasema: Kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyoko Bakkah (Makka), yenye baraka na uongozi kwa ajili ya walimwengu wote Qur(3:96). Tatizo la Waislamu sisi wa leo, hatutaki kubanwa na Model hii ya harakati za Mtume wa Mwenyezi Mungu katika kusimamisha dini ya Allah hapa duniani. Sisi tunataka kubuni dira zetu za harakati, ambazo ni nadharia zaidi kuliko uhalisia. Kama kuna kipengele cha kisiasa na kijamii katika Sunnah, ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu ametuachia kama urithi, basi ni ukombozi wa Makkah. Sijui vipi tunasahau Sunnah hii kubwa kabisa ya Mtume! Ni ukweli usiofichika kwamba mji wa Makkah ndiyo kitovu cha Waislamu duniani. Makkah, ndiko alikozaliwa Mtume, ndiko alikoanza harakati zake, ndiko inakofanyika Ibada ya Hijja, ambayo ni nguzo ya Uislamu, Makkah ni Qiblah cha Waislamu. Ndiyo maana Mtume wa Mwenyezi hakuwa tayari kuiona Makkah ikiwa mikononi mwa Washirikina. Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa na chaguo la kuikwepa Makkah, na kukamata ardhi nyingine kubwa tu, katika eneo la Arabuni au nje ya hapo, lakini hakuzingatia chaguo hilo. Badala yake, aliamua kupambana, kuteseka na kuipigania Makkah kwa hali zote. Hapa kuna funzo kubwa jinsi Mtume alivyodumu katika ajenda muhimu, hata mazingira yakiwa magumu kiasi gani. Hakuhama kwenye ajenda! Alibadili mbinu tu ya kukia lengo, lakini ajenda ni ile ile.
16
AN-NUUR
16
MAULID MUBARAK!
AN-NUUR
Mhariri na watendaji wa gazeti la AN-NUUR wanawatakia Waislamu Sherehe njema za Mazazi ya Mtume (S.A.W.)
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akisalimiana na Muft Sheikh Issa Shaaban Simba. (Picha kutoka Maktaba yetu) Na Mwandishi Wetu SHURA ya Maimamu Mtwara imetoa kauli ikiorodhesha madhila waliyofanyiwa watu wa Mikoa ya Kusini na kusema dhulma sasa basi. Katika kauli hiyo wamesema kuwa katika kipindi cha ukoloni wa Wajerumani (1885-1917), wananchi wa mikoa ya Kusini walitumika kama nguvu kazi ya kuendeleza maeneo mengine yenye migodi na mashamba. Wa k a s e m a , w a t u walinyanganywa ardhi zao na kulazimishwa kuacha familia zao na kwenda Kufanya kazi kwa nguvu katika mashamba ya mikonge mikoa ya Tanga na Kilimanjaro ambapo walikuwa wakijulikana kwa jina maarufu la manamba. Katika sura hii, Mikoa ya Kusini iliachwa bila kuendelezwa ili iwe kitovu cha kutoa wafanyakazi (manamba) wa kutumika katika mashamba ya wakoloni katika maeneo mengine ya nchi. Ushiriki wa watu wa Mtwara katika Vita ya Majimaji ilikuwa ni kielelezo cha kupinga dhulma dhidi yao. Wamesema Masheikh. Wa k i f a f a n u a z a i d i wamesema kuwa ukoloni wa Mwingereza nao uliendeleza dhulma hiyo ambapo Mtwara ilitengwa kama eneo linalostahili kubaguliwa na kuhujumiwa kimaendeleo. Katika utawala wa Wa i n g e r e z a , m w e n d o ulikuwa ni uleule. Mikoa ya Kusini ilitengwa na kubaguliwa kiuchumi. Mwandishi wa Kifaranza Libenow (1971) katika kitabu chake Colonial Rule and Political Development in Tanzania: The Case of Makonde ukurasa wa 11 anaandika kwamba waingereza waliita Mtwara kuwa ni Cinderella Region of a Cenderalla Territory
wa Mtwara wameshuhudia kiwanda cha samaki Mtwara kikiondolewa na kupelekwa Dar es Salaam (na) wameshuhudia taa za mwanga mkali za uwanja wa ndege Mtwara zikingolewa na kupelekwa Arusha. Ni katika hali hiyo Masheikh hao wanasema kuwa wanaungana na wananchi wa Mtwara kupinga gesi asilia kupelekwa Dar es Salaam. Katika kutilia mkazo madai yao wakanukuu maandiko matakatifu wakisema kuwa Kwa hakika MwenyeziMungu anaamrisha uadilifu, na kufanya ihsani, na kuwapa jamaa (na wengineo), na anakataza uchafu na uovu, na dhuluma. Anakunasihini ili mpate kufahamu (mfuate) (Quran 16:90) Na kwamba amesema Mtume (s.a.w) kuwa mwenye kuuona uovu, basi na auondoshe kwa mkono wake, kama akishindwa basi atumie ulimi wake kushajiisha uovu uondoke na akishindwa, basi achukie moyoni mwake na huko kuchukia ni udhaifu wa imani. (Bukhari na Muslim) Wa k a h i t i m i s h a wakisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa muda mrefu wamekuwa wakichukia tu mioyoni mwao maovu na madhila yote waliyokuwa wakifanyiwa na serikali, lakini sasa imefika wakati tuseme na tudhihirishe maovu hayo waziwazi ili asaa viongozi wajirekebishe na wawafanye uadilifu.
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.