Você está na página 1de 3

Statement of Zitto Kabwe published on JamiiForums

SWAHILI
Ndugu zangu. Nadhani ni hekima kujua Jambo kwa kina kabla ya kuanza kulitolea maneno na hukumu. Ninaomba kuelewa kifupi sana nini kilitokea huko twitter. Kuna mama anaitwa Sarah. Mwingereza ambaye pamoja na mume wake waligombana na Benjamin Mengi kuhusu mashamba yanayoitwa sasa Silverdale Farms. Ugomvi huu ulikuwa mkubwa na kuripotiwa mpaka katika Bunge la Uingereza. Huyu mama sasa hivi ameufanya Ugomvi ule binafsi na wa kibiashara kati yake na kina Mengi kuwa ni Ugomvi dhidi ya Watanzania wote. Amekuwa akiandika makala mbalimbali za kuichafua Tanzania. Amekuwa akitaka Serikali ya Tanzania imlipe yeye na mumewe fidia kwa makosa ya raia mmoja wa Tanzania anaitwa Benjamin Mengi. Huyu mama na mumuewe hakuwahi kujiandikisha TIC ili kujua uwekezaji wake kwenye shamba na hata kupata protection ya kisheria. Sasa juzi kaandika makala kuhusu aid dependence ya Tanzania (Jambo ambalo ni la kweli) lakini akaweka takwimu nyingi sana za uwongo ambazo Watanzania wamezidaka na kuzizungumza Kama za kweli hivi. Baadhi yetu tukamwambia through twitter kwamba takwimu sake sio sahihi. Pili tukamwambia alipaswa kusema Kama note katika makala yake kwamba yeye ana kesi na Serikali ya Tanzania. Kwamba yeye amekuwa akiilazimisha nchi yake ya Uingereza iinyime muswada Tanzania mpaka hapo Serikali ya Tanzania itakapomlipa fidia! Mimi naongozwa na msimamo wa wazi kabisa kwamba 'right or wrong my country first' na hivyo siwezi kuruhusu mtu, tena mzungu anayejiita mwekezaji kuitukana nchi nchi yangu kwa sababu tu wamerushana na wafanyabiashara wenzake. Tena nikajulishwa kwamba mama huyu analipwa na Yusuf Manji ili kuitumia Ugomvi huu dhidi ya Reginald Mengi katika vita vyao vya kila siku. Hatuweziweka rehani kwa sababu ya magomvi ya watu binafsi. Nimemwambia huyu mama na ninarudia kusema, muswada hii ni sehemu ya kurejesha Mali zilizonyonywa na ukoloni. Nimemwambia huyu mama kwamba hata Waingereza wakitaka kuondoa misaada Yao waondoe na wala hatutakufa kwa kukosa misaada Yao. Nimemwambia hivyo na ninarudia hapa. That's me, what you see is what you get. Huyu aliyeleta hii thread alete mtiririko wote wa mjadala na sio kipande kimoja tu cha mjadala na kuspin atakavyo yeye na wengi humu mmeingia katika mtego wake bila hata kuhoji

ENGLISH

ENGLISH TRANSLATION
My brothers I think it`s better to know something better before starting to make conclusions about it. I would like to know better what was written in the Twitter. There is a woman called Sarah who is a British whom together with her husband quarrelled with Benjamin Mengi over pieces of land now called Silverdale farms. Their differences were big and even reported in the British Parliament. This lady has now turned the differences or conflict to be personal and turned the business conflict between her and Mengi to look like it involves all Tanzanians. She has been writing numerous articles to tarnish the name of Tanzania and Tanzanians. She has been demanding compensation with her husband from the Tanzania Government over a mistake committed by one Tanzanian called Benjamin Mengi. This woman together with her husband never registered with TIC so that they can know her investment in the land in order to get legal protection. Recently she wrote articles on aid dependence by Tanzania, which is true, but she exaggerated the numbers, which was not true and has led to Tanzanians to start discussing them and believing what she wrote to be true. Some of us told her on Twitter that the figures she wrote are not true. Secondly she should have indicated in her article that she has a case with the Tanzanian Government. She should also have indicated that she has been pressurizing the U.K. Government to stop aid to Tanzania until the Tanzanian Government pays her compensation. As for me, I am led by an open policy of whether right or wrong my country (Tanzania) first and as such, cannot allow a person, furthermore a white person who calls themselves an investor to abuse my country because he/she has differed with his fellow businesspeople. I have also been told that this woman is being paid by Yusuf Manji so that she can persist in the conflict she has with Reginald Mengi. We cannot allow being underlooked because of conflict of two people. I have told this woman and I repeat that it here, this issue is about repatriating wealth taken away by colonialists. I have told this woman that even if British wants to stop aid to Tanzania, let them do so as we will not die as a result. I have told her that and I repeat it here and that`s me saying it openly. The one who brought this discussion should print the whole Twitter conversation and not part of it. She has brought it and many of you have been dragged in her trap to spin for her saga without questioning her intention. ENDS

Você também pode gostar