Você está na página 1de 2

1

STATE HOUSE ZANZIBAR


OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar

21.12.2016

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali


Mohamed Shein amezipongeza juhudi zinazochukuliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar
katika kuimarisha sekta za maendeleo.
Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na
aliyekuwa Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dk. Tonia
Kandiero, aliyefika Ikulu kwa ajili ya kumuaga baada ya kupewa majukumu mengine
ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya (AfDB) Kuisini mwa Afrika.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake binafsi kwa kiongozi huyo pamoja
na Benki ya (AfDB) kwa namna inavyotoa ushirikiano wake kwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo hapa nchini.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alieleza kuwa Benki ya (AfDB) imekuwa ikichukua
juhudi za makusudi katika kuhakikisha miradi mbali mbali ya maendeleo hapa
Zanzibar inaimarika na kuendelea kuwasaidia wananchi wote wa Unguja na Pemba.
Alisema kuwa (AfBD) siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
Zanzibar inapata mafanikio katika kuendeleza miradi yake mbali mbali ya maendeleo
ya kiuchumi na kijamii hivyo, Dk. Shein alizipongeza juhudi hizo ambazo zimekuwa
chachu katika maendeleo ya Zanzibar.
Kwa upande wa uimarishaji wa sekta ya maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk.
Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefaidika kwa kupata mkopo
wenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo ambao utasaidia katika kutatua changamoto
ya uhaba wa maji katika Mkoa huo na si muda mrefu changamoto hiyo itakuwa
historia.
Alieleza kuwa uhaba wa maji umekuwa ni changamoto kwa baadhi ya wakaazi wa mji
wa Zanzibar kwani hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu hapa nchini

2
sambamba na tatizo la tabianchi ambalo linapelekea maji kupungua kwa kiasi kikubwa
katika vyanzo vyake.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alipongeza hatua za Benki hiyo katika kuiunga mkono
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta ya Mawasiliano ya barabara kwa
Unguja na Pemba ambazo zipo zilikuwa zimemalizika pamoja na zile ambazo
zinatarajiwa ujenzi wake kuanza na nyengine kuendelezwa.
Alieleza kuwa miradi ya barabara kisiwani Pemba itasaidia katika kuendeleza sekta
za maendeleo ikiwemo sekta ya utalii sambamba na juhudi nyengine zinazoendelelea
kuchukuliwa na serikali kisiwani humo ikiwemo uimarishaji wa uwanja wa ndege
ambayo nayo itachangia kukua kwa sekta hiyo ya utalii kisiwani humo.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa mbali ya Benki hiyo kutoa ushirikiano wake katika
kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo hapa nchini zikiwemo maji, barabara,
kilimo, nishati, afya, elimu na utawala bora pia, imeweza kutoa mashirikiano katika
nyanja nyengine za kijamii, kiuchumi na kimaendeleo.
Nae aliyekuwa Mwakilishi Mkaazi huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dk.
Tonia Kandiero alimueleza Dk. Shein kuwa Benki yake itaendelea kuiunga mkono
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutambua na kuthamini juhudi inazozichukua
katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.
Dk. Kandiero alipongeza na kusifu mashirkiano mazuri yaliopo kati ya Benki hiyo na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein na kueleza
kuwa hatua hiyo imesaidia sana katika kuleta maendeleo zaidi hapa Zanzibar.
Kiongozi huyo alimuhakikishia Dk. Shein kuwa miradi yote inayosimamiwa na Benki
hiyo itakamishwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara zikiwemo barabara ya
Mahonda -Mkokotoni yenye urefu wa km 31, Fuoni -Kombeni km 8.6, Pale- Kiongele
km 4.6 na Matemwe -Muyuni yenye urefu wa km 7.6.
Pamoja na hayo, Dk. Kandiero ambaye amefanya kazi zake hapa Tanzania kwa
takriban miaka sita, alimueleza Dk. Shein kuwa (AfDB) itaimarisha zaidi uhusiano na
ushirikiano wake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa pongezi za pekee
kwa Dk. Shein na serikali anayoiongoza kwa kusimamia vyema miradi ya maendeleo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Você também pode gostar