Escolar Documentos
Profissional Documentos
Cultura Documentos
TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA
MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY - LITA) KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18
1. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kupitia Wakala wa
vyuo vya Mafunzo ya Mifugo.
2. Katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Serikali kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake
nane; Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke, Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina huduma ya malazi hivyo,
watakaojiunga itabidi wajitegemee. Pia katika Kampasi zetu wanachuo wa ufadhili binafsi watakaopenda kukaa nje ya Kampasi wanaruhusiwa.
3. Wakala inakaribisha maombi kutoka kwa vijana waliomaliza kidato cha nne wanaotaka kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada (Cheti). Pia
vijana waliomaliza Kidato cha sita na wale wenye Astashahada (Cheti) katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba wanakaribishwa kwa ajili
ya kujiunga na mafunzo kwa ngazi ya Stashahada (Diploma).
Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Certificate in Animal Health and Production - CAHP)
6. Sifa za mwombaji
i. Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo (Diploma in Animal Health and Production
DAHP)
Awe amemaliza elimu ya Kidato cha Sita na kufaulu masomo mawili ya Sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Jiografia na
Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha Principal pass moja na subsidiary moja
kwenye masomo ya sayansi. AU
Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Animal Health and Production (AHPC), CAHP NTA level 5, Agrovet au
Certificate in Agriculture and Livestock Production (CALP) waliosoma kwa mfumo wa muhula (term system)
iii. Stashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara ya Veterinari (Diploma in Veterinary Laboratory Technology DVLT)
Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Veterinary Laboratory technology (CVLT) NTA level 5
iv. Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Certificate in Animal Health and Production - CAHP) na Astashahada ya Ufundi Sanifu wa
Maabara ya Veterinari (Certificate in Veterinary Laboratory Technology - CVLT)
Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo mawili ya sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Jografia na Kilimo.
Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha alama ya D kwenye masomo manne,(mawili ya sayansi
na mawili kwenye masomo mengine isipokuwa Dini na Upishi.
AU
Awe amesoma na kufaulu kidato cha nne na kujiendeleza katika vyuo vya ufundi VETA na kupata VTA Level 3 au Trade Test I.
Mtendaji Mkuu,
Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo - LITA,
Veterinari Complex,
131 Barabara ya Nelson Mandela,
S. L. P 9152,
15487 Dar es Salaam